The House of Favourite Newspapers

Kaseke Atimuliwa Singida United

0

 

Deus Kaseke

UONGOZI wa timu ya Singida United, unadaiwa kuwatimua wachezaji wake wawili, Deus Kaseke na Kenny Ally.

Inadaiwa sababu ya kutimuli­wa kwao ni kutokana na utovu wa nidhamu.

 

Habari za kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo, zimedai kuwa Kaseke na Ally waligoma kutoka katika nyumba walizo­pewa wakae kwa muda ambazo walitafutiwa wachezaji wa kimataifa wa timu hiyo waliok­wenda kuzitumikia timu zao.

 

“Timu ilipokuwa Dodoma uon­gozi ulikuwa umewatafutia ny­umba za kuishi wachezaji wote, baada ya kurudi hapa Singida pia ukafanya hivyo ambapo wachezaji wa kigeni walipewa vyumba vyao na wazawa pia walipewa vyumba vyao.

 

“Hivi karibuni baadhi ya wachezaji wa kimataifa walienda kuzitumikia timu zao za taifa ndipo Kaseke na Kenny Ally wakaambiwa na uongozi wakae katika vyumba vile vya wachezaji wa kimataifa na watakaporudi itabidi wawapishe, warudi katika vyumba vyao walivyotafutiwa.

 

“Hata hivyo, baada ya wache­zaji hao wa kimataifa kurudi, Kaseke na mwenzake waligoma kuwapisha, ndipo uongozi ulipokutana jana jioni (juzi) na kuamua kuwatimua katika timu na leo hii (jana) wameondoka kwenda kwao Mbeya,” kilisema chanzo hicho cha habari.

 

Alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, Katibu Mkuu wa Singida United, Abdulrah­man Sima, alisema: “Ni kweli tumewasimamisha kwa muda usiojulikana kutokana na kosa la utovu wa nidhamu na jana (juzi) mchana tumewakabidhi barua za kuwasimamisha.”

Leave A Reply