The House of Favourite Newspapers

Ben Pol Unamdharau Hadi T.I.D?

0
Staa wa Bongo, Ben Pol.

BENARD Paul, maarufu kama Ben Pol, ni mmoja kati ya vijana wanaofan­ya vizuri sana katika muziki wa kizazi kipya, upande wa R&B. Eneo hili lina wakali wengi, lakini kama shabiki wa kweli wa muziki atasema atayarishe orodha yake, sina shaka jina hili litakuwa miongoni mwa majina ya mwanzomwanzo.

 

Kwa waandishi wa habari za burudani wa enzi zangu, wananmchukulia Ben Pol kama kijana aliyejifunza mengi kutoka kwa kaka zake waliomtangulia, halafu yeye akaja kurekebisha makosa yao na kuingiza ubunifu wake, unaomfanya kufikia levo kubwa akiwa bado kinda.

 

Ana sauti ya uanamuz­iki hasa na hata akifanya kolabo na mwenzake, haitii shaka kuhusu kazi itakayo­toka, kwamba itakuwa nzuri na ya kupendeza. Ana nyimbo nyingi kali, ambazo zote zinaweza kuingia katika kuwania tuzo na akashinda.

 

Vibao vyake vya mwan­zomwanzo bado vinagonga vichwa hadi sasa kama Nikikupata, ambacho ndicho kilimtambulisha katika anga la burudani na baada ya hapo, kila mara alipotoa kazi, ilisimama. Nitakukumbusha chache, Maumivu, Sophia na sasa Moyo Mashine, acha zile alizoshirikishwa ambazo zote zimepasua anga vibaya, kama Tatu na Muziki alizo­fanya na Darasa.

 

Katika orodha ya wakali wangu wa muziki huo hapa nchini, ninamuweka daraja moja na Josline, Steve R&B, Marlaw ambao hawa, wanaon­gozwa na kaka zao, Q Chillah na Mnyama TID.

 

Lakini kuna jambo moja limetokea juzikati wakati wa hitimisho za tamasha la kila mwaka la Fiesta, lililofanyika Leaders Club mwishoni mwa wiki iliyopita. Alipopanda jukwaani na kufanya shoo iliyopendeza sana, licha ya kuimba nyimbo zake, lakini pia ali­weka kionjo cha wimbo wa TID, Nyota Yangu.

 

TID hakuwa miongoni mwa wali­opanda juk­waani siku hiyo na kitendo hicho kilim­kera kiasi cha kulipuka hadha­rani kwamba anaangalia uwezekano wa kum­chukulia hatua ‘mdogo wake’ huyo, ili apate haki yake.

 

Nisinge­jali sana

kama baada ya kauli hii ya Mnyama, Ben Pol angeongea kitu cha msingi kumjibu, lakini badala ya kuomba radhi, anaongea kitu kana kwamba ni kawa­ida tu watu kuimba nyimbo za wenzao!

Anatolea mfano wa ‘mbele’ kuwa ni kawaida mtu kuimba nyimbo ya mwenzake na waka­chukulia poa tu. Kwanza nimwambie kuwa siyo kweli kuwa huko mbele anakosema, ambako anamaanisha Ulaya na Marekani, hawaibiani nyimbo kirahisirahisi kama anavyofikiri na kama haelewi, hiyo sheria ya hati miliki imeanzia huko, lengo likiwa ni kuzuia watu kuibiana kazi.

 

Nilimsikiliza akizungum­za wakati akijibu tuhuma za Mnyama. Kwamba aliimba kwa sababu aina ya muziki wanaofanya unain­giliana na kwamba alifanya hivyo kwa vile anam-feel TID tangu akiwa mdogo.

Kama hivi ndivyo, kwamba alikuwa ‘inspired’ na TID tangu akiwa shule, hilo ndilo lilikuwa jambo la kufuatia baada ya kuomba radhi, lakini siyo kama alivyosema kuwa anam­shangaa mkongwe huyo ku-mind wakati ni jambo la kawaida.

 

Kosa kama hili alilifanya

pia Quick Rocka na wenzake wa OMG wakati walipoweka chorus ya Watasema sana. Waliona ni jambo la kawaida tu kwa wasanii. Ben Pol anasema, hata yeye huona bendi zinapiga nyimbo zake katika mabaa na kwamba huko kote ni kopi tu.

 

Msanii wa kawaida anaweza kuona hilo ni jambo la kawaida, lakini siyo kwa msanii anayeji­tambua. Kama angejaribu kurudi nyuma na kuona jinsi kibao hicho cha Nyota Yangu kilivyomsumbua TID wakati akikitoa, asingeona ni jambo la kawaida kuupiga kwenye shoo ambayo yeye amelipwa.

 

Wimbo huu ulipotoka mwaka 2006 kuelekea 2007, kukatokea songombingo la kufa mtu baada ya mtan­gazaji Abdalah Mwaipaya ‘Heavy D’ kupiga nyimbo mbili zilizofanana beat na namna wanavyoimba, wakip­ishana lugha. Moja iliimbwa Kireno na nyingine Kiswahili.

 

Ikadaiwa kuwa TID aliiba nyimbo hiyo kutoka kwa msanii mmoja aliyeitwa Pasada kutoka Msum­buji, kitu ambacho Mnyama alikikanusha hadi mate yalimkauka.

Nimpe mwongozo mdogo wangu Ben Pol, yeye ni mmoja wa wasanii wazuri hapa nyumbani, anafanya vi­zuri katika vibao vyake vingi. Anao uwezo wa kutengen­eza kazi zake na zikatusua kama inavyojionyesha wazi.

Anapohitaji kuingiza kion­jo cha mtu mwingine, hasa katika maonyesho rasmi, siyo jambo baya kufanya mawasiliano naye, kwa sababu katika wakati ambao vyuma vimebana kama hivi, ni rahisi mtu kuamini umefanikiwa katika shoo au wimbo wako kza chembe
Lazima Ukae OJUKU ABRAHAM, +255 719 786 355

 

Leave A Reply