The House of Favourite Newspapers

Aslay na Dogo Janja Waiteka Maisha Basement (Video + Pichaz)

Msanii wa muziki Bongo Fleva, Aslay akifanya yake Usiku wa Ngarenaro ndani ya klabu ya Maisha Basement usiku wa kuamkia jana.
Shoo ikiendelea.
Aliyekuwa memba wa Kundi la Yamoto Bend, Enock Bella (kushoto) akiimba wimbo wa zamani wa kundi hilo sambamba na Aslay.
Nyomi ya mashabiki waliojitokeza Maisha Basent.
Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva, Dogo Janja akitoa burudani.
Mpiga picha mashuhuli katika filamu za Bongo, Farid Uwezo akimtunza Dogo Janja.
Mashabiki wakiendelea kujiachia.
Dogo Janja akimtambulisha Aslay ndani ya Maisha Basement wakati shoo ikiendelea…
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva nchini kutoka Tip Top Connection Madee Ally akitoa burudani.

Usiku wa kuamkia jana kulitisa burudani baada ya wakali wa Bongo Fleva, Aslay na Dogo Janja kufanya shoo ya nguvu katika Usiku wa Ngarenaro ndani ya Ukumbi wa Maisha Basement uliopo Kijitonyama, jijini Dar.

 

Katika shoo hiyo iliyohudhuriwa na mastaa mbalimbali pamoja na nyomi ya mashabiki, ilianza kwa Aslay kupanda jukwaani na kupiga vibao vyake vinavyotamba kuanzia Natamba, Hauna, Likizo na nyinginezo huku shangwe za kutosha kutoka kwa wadada zikiliteka jukwaa.

Baada ya kushuka Aslay, Mkali Janjaro naye alipanda na kukamua shoo ya nguvu kupitia vibao vyake vinavyotikisa kama vile My Life na Ngarenaro vilivyowakosha mashabiki wengi.
Miongoni mwa mastaa waliotoa sapoti katika shoo hiyo alikuwemo Aunty Ezekiel, Wema Sepetu, Steve Nyerere, Rammy Gallis, Madee na Wengine kibao.

Comments are closed.