The House of Favourite Newspapers

Jamani Antiii…Nishushe Ununio-13

“Baby…” aliita Vivian wakati huohuo mkono wake wa kushoto ukikiparamia kifua cha fundi kilichokuwa wazi na kuiacha bustani ionekane kwa uwazi na ukubwa wa kumezesha mafunda ya mate.

Vivian hakuishia hapo, akakiruhusu kiganja kutembea bustanini kwa Bigambo huku vidole vyake laini vikitalii ambapo maruhani ya Bigambo yalikuwa.

“Mmm…,” aliguna Bigambo kwa mtindo wa kufyonza muwa mtamu…

“Oooh, yes baby…,” Vivian alichombeza kwa maneno laini na kuyafumba macho kwa maana ya kuhamasisha zaidi. Hali ya Bigambo ikazidi kuwa mbaya, kama ni kuharibikiwa sasa ilikuwa kwa kiwango cha kuhitaji msaada kamili na si maneno matupu.

Kuona hivyo, Vivian akazidisha mbwembwe. Akafumba macho na kukisogeza kinywa karibu na kile cha Bigambo. Bigambo naye akalegea kwa maana ya kumpokea Vivian kwa mtindo huo. Wakasogeleana na kuanza kushiriki pamoja kutafuna miwa ya Kilombero.

TWENDE PAMOJA SASA…

Kufumba na kufumbua, Vivian alijiweka sawa tayari kwa kuruhusu mechi ianze kuchezeka. Kuona hivyo, Bigambo alijiweka sawa na kumgeukia Vivian. Akanyoosha mikono na kuyaparamia maembe mawili na kufanya kama anayebonyeza ili kuona kama yameiva na yanafaaa kwa kuliwa.

Vivian aliruka na kutoa kilio kilichomfanya Bigambo aangue kicheko cha nguvu.

“Unacheka nini sasa jamani,” Vivian alilalamika huku akijinyonga kiaina, staili ya kumshika kwenye matunda aliyoitumia Bigambo ilikuwa ni ya kipekee mno, kiasi cha kumchanganya vilivyo Vivian, mwanamke kutoka Mbeya mwenye umbo na muonekano matata kabisa machoni kwa kila mwanaume rijali mwenye kujua matumizi sahihi ya watu wa aina hiyo.

“Kwani kucheka ni dhambi jamani V?” Bigambo alijibu swali la kwa nini alikuwa akicheka, lakini hakuishia kwa kujibu swali pekee badala yake alipeleka tena mkono na awamu hii alizungusha hadi sehemu ya nyuma ya Vivian, juu kidogo ya lile eneo la kukalia na alitumia vizuri vidole vyake alijikuta akishika vitu vigumu vilivyopangwa kwenye mstari maalum.

“Aaah, wewe B…!” Vivian alizidi kulalama akijitingisha palepale kitandani, wakati huo chupa za bia vinywaji vyao vilikuwa bado mikononi, kwa maana kwamba utundu wote aliokuwa akiufanya Bigambo kwa Vivian, alitumia mkono mmoja kuleta mateso hayo yote.

Ikafika mahali Vivian akaanza kujisikia vibaya sana. Lile agano la kutofanya chochote pindi wakifika ndani lilianza kuyeyuka ubongoni na sasa mwili wake ulianza kuhitaji kushikwashikwa kwa maeneo yaliyohitajika kushikwa.

“Lakini kumbuka ahadi yetu Bigambo,” Vivian alichombeza kutoka moyoni, maneno hayo hakumaanisha, bali ilikuwa ni ile hali ya kujitetea heshima yake asionekane kulegea kirahisi.

“Ahadi gani tena…?” Bigambo aliuliza akiweka chupa ya kinywaji mezani na kumtazama mzimamzima Vivian ambaye naye aliweka chupa ya Savanna mezani na kubaki kimya akimtazama Bigambo kwa lile jicho la pembeni na kusindikiza kwa tabasamu laini na kuyaacha meno yake ya mbele yaliyoungua kidogo yaonekane sawia kwenye mboni za macho ya Bigambo.

“Si hatufanyi?”

“Nini?

“Haa, jamani kwani wewe si unajua kabisa mwanaume na mwanamke hufanya nini wanapokutana chumbani wakiwa wawili na kama hawana undugu wowote?”

“Mimi sijui, kwani humu tumekuja kufanya nini?”

“Bigambo bwana, hebu acha mambo yako…”

“Mambo gani tena…?”

“Wewe si umesema tunakuja kuzungumza kwa uhuru?”

“Sasa si ndiyo hivi au kuna uhuru zaidi ya kuzungumza hivi?”

“Sawa, lakini nasisitiza tu kwamba tusifanye chochote.”

“Nimekuelewa, lakini tunaruhusiwa kugusana kwa maana ya kukushika mfano mkononi au kichwani…?”

“Yaani wewe, sasa kunishika huko kichwani unatafuta nini kama siyo uchokozi wa kuamsha mambo mengine ya kuwekana majaribuni?”

“Noo, si naweza mfano kuwa nasifia unadhifu wa nywele zako jinsi zilivyolala kwa mpangilio mzuri?”

Hapo sasa Vivian alinyamaza lakini kunyamaza kwake kulikuwa ni kujiuliza mara mbilimbili kama akaze kikwelikweli au alegeze kiaina na mchezo baina ya Yanga na Singida United ichezwe na kila mmoja aondoke zake.

“Haya bwana, siwezi kukuzuia maana una maneno mengi kama mbunge wa kuteuliwa…,” Vivian alianza kulegeza na kujiachia kiuhuru sasa, lakini hakuacha kusisitiza kutofanya mchezo wa maigizo wafanyao watoto wadogo wanapocheza.

“Sibadili msimamo wangu, hatufanyi…,” alikazia Vivian huku akijiachia kwa kulala chali kitandani, ingawa hakuwa amevua nguo yoyote. Kitendo cha kulala chali kulisababisha eneo la mbele kuonekana vizuri kitendo kilichomfanya Bigambo alambe midomo kwa ubembe wa kimahaba na uchu.

“Ila…,” Bigambo alisema na kuishia njiani.

“Ila nini tena Bigambo…?”

“Umependeza sana…”

“Kwa lipi?”

“Mfano hili hapa eneo la mbele…,” Bigambo alisema huku akiweka mkono wake wa kulia juu ya kisima cha burudani.

“Ooh, wewe Bigambo jamani…,” Vivian aligutuka na sasa aliinuka na kulegea zaidi, ambapo alilala tena na kunyoosha miguu yote, lakini Bigambo hakuondoa mkono wake eneo hilo na badala yake alianza kutumia utundu zaidi kwa kupapasa kwa mikogo, hali iliyomfanya Vivian arukwe na akili, mwisho wa siku aliamua liwalo na liwe.

Sasa alimgeukia vizuri Bigambo na yeye kumrushia mashambulizi. Alianza kushika maeneo mbalimbali, hali iliyomfanya Bigambo kuanza kujikunja na kuwewesekea kitendo hicho. Ikafika mahali hakuna aliyewaamuru wachojoe magwanda yao lakini kila mmoja alijikuta akijiamrisha mwenyewe.

Joto la miili yao lilikuwa limepanda na kufikia kiwango ambacho kama ni mgonjwa wa malaria hali ilikuwa mbaya sana. Wote walibaki kama walivyokuja duniani na Bigambo alimfuata Vivian.

Bigambo alipeleka kinywa hadi kwenye papi za mdomo wa Vivian, ambaye midomo yake ilikuwa na lipsi nene na zenye kuvutia zaidi. Vivian alilala kwa mtindo wa kuhesabu mabati, Bigambo kuona hivyo, akiongozwa na mhemko wa kilevi alichokuwa ameshindilia, alianza kuyakabili matunda ya mwanamke huyo ambaye kwa wakati huo alikuwa akihema kama bata dume aliyetoka kupambana na mwenzake.

Hakuishia hapo. Bigambo alitoa ulimi na kuanza kufanya utalii kwenye maeneo mbalimbali ya mwili wa Vivian aliyekuwa akiendelea kuhema huku akifumba na kufumbua macho. Ulimi wa Bigambo ulianza na eneo la juu ya kila tunda la Vivian, sasa ilikuwa ni zamu ya vile vikonyo viwili kabla ya kuhamia chini yake, mahali ambapo matunda mawili yalikuwa yamelalia.

Vivian aliendela kujitikisa kwa kufuatisha msisimko uliotokana na utalii wa ulimi wa Bigambo mwilini mwake. Ikafika mahali ulimi ukavuka mipaka, kitendo kilichomfanya Vivian kuanza kuropoka.

“Bigambo…”

“Naam…”

“Unajua sana jamani baba.”

“Kufanya nini?”

“Kunipa raha, unaniweza sana jamani…,” Vivian alijieleza kwa maneno yote matamu aliyoyajua lakini Bigambo hakusitisha suluba zake ambapo sasa alianza kutumia jembe lake kumuadhibu Vivian.

Ikafika mahali alishika jembe lake na kuanza kulima kwa fujo zote kama vile kibarua aliyeoneshwa pesa na kuambiwa anza kulima na umalize ndani ya nusu saa, alianza na eneo la mgongo, kabla ya kushuka kiunoni na kuyagusa mapingili ya nyonga.

Vivian alishindwa kuvumilia, bila kuamrishwa alijiweka sawa mwenyewe na kumtaka Bigambo aanze kulima shambani kwake kwani msimu wa mvua ulikuwa umeshaanza na maji yalikuwa ya kutosha kwa mpunga kustawi vizuri. Bigambo hakuona shida kufanya hivyo, sasa alijiweka mkao mzuri wa kulima kwa ustadi shambani kwa Vivian.

Mtanange ulikuwa wa kukata na shoka. Timu zote mbili zilikuwa zikishambulia lango la timu pinzani kwa nguvu na pasi za kushtukiza. Ikafika mahali Vivian alichoka na kuruhusu mashuti kadhaa yatikitise nyavu za golini kwake.

Dakika 47 baadaye, wote wawili walijikuta wakitangaza kufika mwisho wa miti ya minazi na sasa walialikana kupasua madafu pamoja. Kwa upande wa Bigambo lilikuwa dafu lake la kwanza kupasua tangu waanze kazi ya kukwea minazi lakini kwa upande wa Vivian lilikuwa kama dafu la nne na viungo vyake vyote vilikuwa hoi hususan miguu ambayo hutumika zaidi kwenye zoezi la ukweaji wa minazi.

“Nafika…,” Vivian alianza kutangaza kwa sauti ya kupayuka huku akihangaika mwili mzima ili ashike vizuri asije akaanguka na badala ya kuvunja dafu iwe stori nyingine.

“Umefika wapi mama…?” Bigambo alihoji lakini kabla hajajibiwa naye alianza kusikia kitu cha tofauti na sasa alianza kukoroma huku akikunja sura na hapohapo alianza kuropoka kwa sauti yake ile mbaya.

“Oooh, mama nami naelekea kupasua daaaafuuuu…,” Bigambo aligugumia na hapohapo alizidisha kasi ya ukweaji na kulishika dafu moja kabla ya kuliachilia na kulipasua kwa hasira kali, kitendo kilichomfanya Vivian naye apasue la kwake wote kwa pamoja walijikuta wakihitimisha safari kwa wakati mmoja, lakini kufumba na kufumbua Vivian alianza kuonesha jambo ambalo hata Bigambo lilimshangaza kwani hakulitegemeaa, lakini wakati huohuo mlango ukawa unagongwa kwa fujo kali sana.

Je, nini kitafuata? Usikose kufuatilia Jumamosi katika Risasi Jumamosi. 0673 42 38 45.

Comments are closed.