The House of Favourite Newspapers

Dotnata: Nimepona, Sasa Ni Kazi Tu

Staa wa kitambo wa Bongo Movies, Illuminata Poshi ‘Dotnata’.

BAADA ya kukaa kimya kwa muda mrefu kutokana na kupata ajali ya kuteleza na kuanguka nyumbani kwake ambapo alivunjika mguu, staa wa kitambo wa Bongo Movies, Illuminata Poshi ‘Dotnata’ ameibuka na kusema kwa sasa amepona, anachofanya ni kufanya kazi kwa bidii.

 

Akizungumza na Za Motomoto News, Dotnata alisema kuwa, alikaa muda mrefu bila kujihusisha na sanaa kwa sababu ya kuugua, lakini kwa sasa anamshukuru Mungu amepona na anaweza kutembea vizuri hivyo ameanza kushuti tamthiliya.

 

“Siwezi kuiacha sanaa maana ninaipenda na nilikaa kimya kwa sababu ya kuumwa, lakini nimepona sasa, nawaomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwani nakuja na tamthiliya kali kwani kwa sasa filamu hazilipi ila hizo tamthiliya ndiyo zinalipa mno,” alisema Dotnata.

STORI: GLADNESS MALLYA | RISASI MCHANGANYIKO

Comments are closed.