The House of Favourite Newspapers

Museveni Akubaliana Na Trump ‘Kuwananga’ Waafrika

Rais wa Marekani, Donald Trump.

RAIS Yoweri Museveni wa Uganda amesema anampenda Rais wa Marekani, Donald Trump, kwa kusema ukweli baada ya kuzishambulia baadhi ya nchi duniani zikiwemo za Afrika ambazo alisema ni “chafu”.

 

Rais Yoweri Museveni wa Uganda

“Anawaambia Waafrika ukweli,” alisema Museveni baada ya kauli hiyo ya Trump ambayo ilishutumiwa sehemu mbalimbali duniani ikiwemo Afrika.  MusevenI alisema hajui kama Trump alinukuliwa vibaya, hata hivyo hilo si tatizo kwani rais huyo husema ukweli, na mtu hawezi kuwa imara iwapo ni mnyonge.

Rais wa Ghana, Nana Akufo-Addo (kushoto) na Rais wa Namibia, Hage Geingob, walioshutumu maneno ya Trump kuhusu Afrika.

Viongozi kadhaa wa Afrika wakiwemo marais Nana Akufo-Addo wa Ghana na Hage Geingob wa Namibia, walishutumu lugha hiyo.

 

Trump alitumia maneno hayo akiwa ikulu ya Marekani, Januari 12, mwaka huu ambapo yalishutumiwa na baadhiya watu kuwa ni ya “kibaguzi, ya kushitua na ya aibu”.

WALUSANGA NDAKI/MITANDAO/MASHIRIKA

Comments are closed.