The House of Favourite Newspapers

Lulu Diva Jeuri Hii Kaipata Wapi?…Anaishi Kwenye Mjengo wa Kifahari

Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’.

WAKATI wasanii wengine wakilia njaa kali sambamba na kuwa na maisha ya kawaida, hali ni tofauti kwa msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ambapo kwa sasa maisha yake yameonekana kumnyookea baada ya kunaswa akiishi kwenye mjengo wa kifahari pande za Mbezi Beach jijini Dar.

Akisonga ugali.

Gazeti hili kwa mara ya kwanza limefanikiwa kuunasa mjengo huo wa kifahari ndani ukiwa na vivutio mbalimbali.

KAUNTA ZA VINYWAJI

Ndani ya mjengo huo una kaunta mbili maalum kwa vinywaji laini ambapo ya kwanza ipo sebuleni na ya pili ipo jikoni huku pia kukiwa na friji kubwa la kisasa la milango miwili lenye thamani ya mamilioni.

…Akifungua Friji lenye mapochopocho.

SEBULE YA KISASA

Ukiachana na sofa na fanicha za kisasa, upande wa sebuleni umepambwa kwa ‘wallpaper’ za aina yake sambamba na nakshinakshi kwenye meza maalum iliokaa mfano wa ‘dressing table.’

 

ENEO KUBWA LA PARKING

Upande wa nje kuna eneo kubwa la parking la kisasa lililo ndani ya uzio ambapo eneo hilo unaweza kuhifadhi magari zaidi ya matano.

GARI LA KIFAHARI

Ukiachilia mbali ndani na nje ya jumba hilo, Lulu Diva pia anamiliki gari jeusi la kifahari aina ya Jeep ‘Liberty’ toleo la Marekani.

…Lulu diva akipata chakula cha mchana.

AMETOA WAPI JEURI?

Licha ya kuendelea kusumbua na kuwa msanii mwenye mafanikio kwa sasa, Lulu ni miongoni mwa wasanii wa Bongo Fleva walioanza rasmi muziki mwaka jana akiwa ameshikilia ngoma tatu hadi sasa, Usimuache, Utamu na Give It To Me.

…Akiwa mbele ya gari na nyumba anayoishi.

Awali alikuwa akiuza sura kwenye muziki huo, swali la kujiuliza amepata wapi jeuri hii?

Katika kumdodosa, Lulu Diva amesema ana siri nzito kuhusu maisha yake bomba anayoishi sasa hivyo akaomba subira kabla ya kumuanika anayempa jeuri mjini.

STORI NA IMELDA MTEMA | GAZETI LA IJUMAA | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.