The House of Favourite Newspapers

20 Wakamatwa Kwa Kula Mchana Mwezi Wa Ramadhan

Jeshi la Polisi wa Kiislamu (Hisbah) katika Jimbo la Kaskazini Nigeria la Kano, wamewakamata waumini wa dini ya Kiislamu waliokutwa wakila hadharani mchana pamoja na wale waliokuwa wakiwauzia chakula katika siku za mwanzo za Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.

Naibu Kamanda wa Hisbah, Mujahid Aminudeen ameliambia Shirika la Habari la BBC kwamba watu 20 walikamatwa kwa kula mchana huku wengine watano wakikamatwa kwa kuuza chakula na kueleza kuwa oparesheni hizo zitaendelea kwa muda wote wa mwezi wa Ramadhan.

“Ni muhimu kutambua kuwa hatujishughulishi na wasiokuwa Waislamu, kutouheshimu mwezi wa Ramadhan haikubaliki,” alisema Mujahid.