The House of Favourite Newspapers

2017 Ni Full Vicheko, Vilio Kwao!

 Babu Seya (kulia) na Papii Kocha wanamuziki hawa wawili hawataisahau baada ya Rais John Magufuli kutangaza msamaha kwao.

MWAKA 2017 ndiyo unaelekea ukingoni huku ukiacha alama mbalimbali kwa watu maarufu, ambao utabakia katika historia yao. Na siyo mastaa tu, kwani hata watu wengine wa kawaida nao mwaka unayoyoma ukiwaachia maumivu na furaha kila mmoja kwa wakati wake.

 

Katika kundi la mastaa, mwaka huu kulikuwa na matukio ya kusikitisha kwa baadhi yao, huku wengine wakiachia tabasamu au kicheko kutokana na mambo yao kuwa supa.

Katika makala haya tunakuletea orodha ya baadhi ya mastaa ambao wanamaliza mwaka huu wakiwa wanacheka na wengine wakiwa wamenuna kutokana na matukio mbalimbali yaliyotokea.

Staa wa Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

 

 

BABU SEYA NA PAPII KOCHA

Desemba tisa mwaka huu, wanamuziki hawa wawili hawataisahau baada ya Rais John Magufuli kutangaza msamaha kwao kufuatia hukumu dhidi yao ya makosa ya kubaka iliyowafanya wafungwe jela kifungo cha maisha.

Kwa zaidi ya miaka 13, wanamuziki hao walikuwa gerezani wakitumikia kifungo chao, huku juhudi zote za kukata rufaa katika mahakama za ngazi zote nchini kugonga mwamba na hivyo tumaini pekee walilobaki nalo ilikuwa ni Mungu pekee.

Mwanamuziki Zuwena Mohamed.

ZUWENA MOHAMED ‘SHILOLE’

Mwaka huu unamalizika vizuri kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, ambaye jina lake halisi ni Zuwena Mohamed lakini maarufu kama Shilole.

Baada ya kuandamwa na skendo ya kupenda kujihusisha kimapenzi na wanaume wenye umri mdogo kuliko yeye, hatimaye mwaka huu aliamua kukata mzizi wa fitina kwa kufunga ndoa na kiben’ten wake, Ashrafu Uchebe.

Ukiacha ndoa hiyo, pia Shilole ambaye pia ni mjasiriamali, alifanikiwa kufungua mgahawa wake unaojulikana kwa jina la Shishi Food ambao ni chanzo kingine cha kipato ili kukabiliana na ukata ambao wengi wanalia wakisema vyuma vimekaza.

HADITHI: SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU – SEHEMU YA 1 (Audio)

Nakuletea dakika 15 za kwanza za simulizi hii tamu ya SIKU ZA MWISHO ZA UHAI WANGU. Ukitaka kuisikiliza simulizi hii Install #GlobalPublishersApp sasa. Utasoma na kusikiliza kitabu chote kuanzia sehemu ya kwanza hadi ya mwisho bureeeee!

Android: Bofya ==>http://bit.ly/2AAQe1d
iOS: Bofya ==>http://apple.co/2Assf4M

ASLAY ISIHAKA

Dogo alianza kama utani wakati ule akiwa chini ya lebo ya Mkubwa na Wanawe alipoibuka na kibao chake cha Nakwenda Kusema. Taratibu akafanya vizuri akiwa na bendi ya Ya Moto kabla ya kujitoa na kuanza kufanya kazi kivyake.

Mwaka huu unamalizika ukimuacha akiwa mwenye furaha kubwa kwa sababu ni miongoni mwa wasanii waliofanya vizuri baada ya kuachia ngoma tatu mfululizo ambao zote zilikuwa ‘hit’, zikibamba kila kona.

Alikuwa mmoja kati ya wanamuziki waliofanya vizuri katika tamasha kubwa la kila mwaka la Fiesta, ambalo lilihitimisha safari yake ya mikoa mbalimbali nchini jijini Dar es Salaam.

 

Staa wa  Filamu, Irene Uwoya.

IRENE UWOYA

Mwaka huu hauwezi kutoweka katika kumbukumbu za Irene Uwoya baada ya aliyekuwa mumewe, Hamad Ndikumana ‘Kataut’ kufariki dunia ghafla jijini Kigali Rwanda.

Ulikuwa ni msiba mzito hasa kufuatia sintofahamu iliyosababishwa na filamu aliyocheza na Dogo Janja kuwafanya baadhi ya watu, akiwemo mumewe huyo, kuamini kuwa ilikuwa ni ndoa ya kweli.

Staa wa filamu Wema Sepetu

WEMA SEPETU

Mwaka huu unayoyoma ukimuacha Wema Sepetu akiwa mwenye majonzi moyoni mwake, hasa kufuatia msala wa kukutwa na ‘ganja’ nyumbani kwake, ambao hivi sasa unamfanya kuwa na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar.

 

ELIZABETH MICHAEL ‘LULU’

Kwa kila hali, huu ni mwaka ambao utakaa kichwani mwa Lulu kwa miaka mingi, kwani unamalizika ukimuacha akiwa si rafiki tena, baada ya Mahakama Kuu kumtia hatiani na hivyo kumhukumu jela miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia.

 

Lulu alikuwa na kesi ya kumuua mpenzi wake, ambaye pia alikuwa ni muigizaji, Steven Kanumba, katika tukio lililotokea nyumbani kwa marehemu, Sinza Vatican.

Comments are closed.