The House of Favourite Newspapers

“2018 Ulikuwa mwema kwangu” Vanessa Mdee

 

SEXY lady anayefanya poa kunako gemu la Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’amesema kwa upande wake mwaka 2018 ulikuwa mwema na anamshukuru Mungu  amemfikisha salama mwaka 2019.

 

Akipiga stori na Ijumaa Showbiz, Vanessa alisema mwaka 2018 alitimiza baadhi ya ndoto zake ikiwemo kuzindua albam yake ya Money Mondays na viatu vyake ya Bora Star by Vanessa Mdee.

 

“Mwaka 2018 ulikuwa poa sana kwangu, namshukuru Mungu nilitimiza baadhi ya ndoto zangu ikiwemo kuzindua albam yangu ya Money Mondays na viatu vyangu vya Bora Star by Vanessa Mdee, naomba Mungu azidi kunifanikishia zaidi na zaidi mwaka 2019,’’ alisema Vee Money ambaye ni mchumba wa msanii Juma Jux.

Comments are closed.