The House of Favourite Newspapers

Tambwe: Sikujua Tatizo Langu ni Zito

Amissi Tambwe

BAADA ya kufanyiwa upasuaji mdogo wiki iliyopita na kulazimika kupumzika, Amissi Tambwe anasubiri kuondolewa nyuzi tu kwenye goti. Tambwe alifanyiwa upasuaji huo baada ya kuwa anasumbuliwa na goti kwa muda mrefu tangu msimu huu uanze jambo ambalo limekuwa likimuweka nje na kuigharimu Yanga.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Tambwe alisema; “Sikujua kama tatizo langu lilikuwa ni kubwa ndiyo maana nikawa nacheza tu lakini naendelea vyema kwa sasa nachosubiri ni kutoa zile nyuzi baada ya hapo nitapata maelekezo kutoka kwa daktari.”

 

“Naomba tu mambo yaweze kwenda sawa nirejee uwanjani kwa mara nyingine sababu msimu huu kwangu umekuwa ni wa changamoto lakini naamini nitapona na kuendelea kupambana. “Nipo kwenye kipindi kigumu lakini ndiyo changamoto zenyewe za mpira,” alisema Tambwe ambaye aliwahi kuichezea Simba.

STORI NA MARTHA MBOMA

Comments are closed.