The House of Favourite Newspapers

Mwalimu Kashasha Awabonyeza Simba

Wachezaji wa timu ya Simba wakishangilia.

MCHAMBUZI mahiri nchini, Alex Kashasha ‘Mwalimu Kashasha’ ameweka wazi kuwa Simba ina uwezekano wa mkubwa wa kuchukua ubingwa wa msimu huu kwa asilimia sitini iwapo haitofanya uzembe wa kubweteka.

 

Licha ya kushiriki michuano ya kimataifa, Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 46, Yanga wanashika nafasi ya
pili wakiwa na pointi 43 wakifuatiwa na Azam wenye pointi 41, wote wakiwa wamecheza michezo 20 hali inayofanya ushindani wao kuwa mkubwa.

 

Akizungumza na Spoti Xtra ambalo ni gazeti linalonunuliwa na kusomwa zaidi kila Jumapili, Kashasha alisema Simba wana nafasi kubwa sana lakini Yanga ikicheza karata zake inaweza kupindua meza.

 

“Kiukweli kwa namna Simba walivyosimama msimu huu wana asilimia sitini ya kuchukua ubingwa kutokana na mtaji mkubwa wa mabao waliokuwa nao, wakifanya uzembe wa aina yoyote au wakajiachia wakakutwa na Yanga kwa maana ya mabao itakuwa ngumu kwao. “Lakini uwezo wa wao kuchukua ubingwa kwa upana wa kikosi chao ni mkubwa ndani ya msimu huu.

 

Wachezaji kama wataendelea kufanya mzunguko wa kubadilishana kucheza wote kwa sababu kumekuwa na shida kwenye nchi hii kwamba timu nyingi wanasajili wachezaji 30 lakini unakuta wanaocheza ni 12, 13 au 14.

 

“Sasa kukitokea majeruhi ndiyo mtu sasa anaonekana kucheza kama ilivyotokea kwa Azam baada ya Razak Abalora kupata matatizo ndiyo Mwadini Ally ameanza kucheza, sasa kama watatumia vizuri wachezaji hakutakuwa na cha kuwazuia kuwa mabingwa,” alisema Kashasha ambaye mbwembwe zake za lugha kwenye uchambuzi zinawakosha mashabiki.

 

MKUDE ANENA Akizungumza na Spoti Xtra, Mkude alisema; “Tumejiandaa kufanya vyema katika kila mechi tutakayocheza hivi sasa, Yanga kubakisha pointi tatu kutufikia ndio mpira ulivyo, lakini wasitarajie kuwa wataweza kutupita.” Mkude alisema wana matumaini ya kumaliza ligi vizuri kutokana na kujituma kwao

Comments are closed.