NI mmoja kati ya wachezaji ambao wamekuja na kuweza kuinusuru Lipuli FC ambayo ni wazi licha ya kupambana lakini jahazi lake lilikuwa na dalili ya kuzama kutokana na safu ya ushambuliaji kuonekana kuwa butu.
Hii ni kutokana na Lipuli kupata pigo la kuondokewa na beki wake mahiri, Mghana, Asante Kwasi ambaye alikuwa msaada katika upachikaji mabao ambapo mpaka anakwenda Simba alikuwa amefunga mabao matano na sasa Lipuli imefunga jumla ya mabao 16 kwenye mechi 22 za Ligi Kuu Bara.
Baada ya k u o n d o k a , timu hiyo ilitumia dakika 540 ambazo sawa na mechi tano kuweza kufunga tena bao a m bapo waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Stand United.
Huyu si mwingine bali ni mshambuliaji Adam Salamba ambaye anaonekana kama ndiye anayeibeba Lipuli kwa sasa kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao tangu asajiliwe kipindi cha dirisha dogo.
S a l a m b a a m e f a n i k i w a kucheza mechi nane tangu asajiliwe kipindi cha dirisha dogo na amefunga mabao matano kwenye michezo hizo.
Haya ni sehemu ya mahojiano kati yake na Championi Ijumaa ambapo anaelezea masuala yake ya soka.
ULIANZIA WAPI KUCHEZA SOKA?
“Soka la ushindani nilianza kucheza mwaka 2014 nikiwa timu ya Ligi Daraja la Pili inayofahamika kwa jina la Bulyanhuru ya Shinyanga ambayo ilikuwa ikidhaminiwa na Kampuni ya Acacia.
“Lakini nikiwa hapo niliitwa timu ya Maboresho ya Vijana U-23 na Kocha Mart Nooij na Salum Mayanga.
“Baada ya hapo nilibahatika kusajiliwa na Geita Gold, ulikuwa msimu wa mwaka 2015/16, nilicheza pale lakini mechi moja pekee tukaanza kusumbuana kwenye suala la malipo na timu ilikuwa ipo Ligi Daraja la Kwanza, hivyo nikaachana nao.
“Nikatimkia Zanzibar kwenye kikosi cha Polisi Zanzibar, hapo nilicheza nusu msimu nikaamua kuondoka, nikaenda kufanya majaribio Mtibwa Sugar, kwa bahati mbaya walimu wa pale hawakunielewa, ikabidi niondoke tu.“Nikarudi Shinyanga kwenye timu yangu ya Bulyanhuru wakati huo nikawa nasubiri dirisha kubwa lifunguliwe.
ILIKUWAJE UKATUA STAND UNITED?
“Nilikwenda Stand United kufanya majaribio kipindi cha ‘pre-season’ bahati nzuri nilikutana na yule kocha Mfaransa, Patrick Liewig, alikubali uwezo wangu, nikawa nimesajiliwa hapo.
“Msimu uliopita ndiyo nilianza kuichezea Stand United, bahati nzuri mechi ya kwanza tulicheza na Azam FC pale Kambarage nikitokea benchi nilifanikiwa kufunga bao moja ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo, nilifurahi sana sababu ilikuwa mara ya kwanza kucheza ligi kuu na nimefanikiwa kuifunga timu kubwa kama Azam.
“Lakini katika mzunguko wa kwanza nikiwa na Mfaransa sikuweza kupata sana nafasi ya kucheza zaidi nilikuja kupata kwenye raundi ya pili baada ya Kocha Hemed Morocco kuanza kuinoa Stand na mpaka msimu unaisha nilifunga mabao manne pekee.
TUKIO GANI LILIWAHI KUKUUMIZA KATIKA SOKA?
“Na k umb u k a baada ya kuihama Stand na kutua Lipuli, tulipocheza
kulipwa wakasahau kabisa fadhila na kuweza kunifanyia vile jambo ambalo si zuri.
TOFAUTI KATI YA STAND NA LIPULI NI IPI?
“Tofauti ipo kubwa, nilipokuwa Stand nilipewa majukumu mengi ndiyo maana haikuwa rahisi sana kuweza kufunga mabao sababu straika nilikuwa mwenyewe.
“Upande wa Lipuli nimepewa jukumu la kufunga tu ambapo nimekuwa nikisaidiana na wenzangu, ndiyo maana inakuwa rahisi kuweza kufunga.
CHANGAMOTO IPI UMEPATA MSIMU HUU?
“ Kwa n z a kitendo cha mimi kutua Lipuli FC ulikuwa ni mtihani m k u b w a sana kwangu hasa kimazingira, awali nilipata shida kutokana na baridi, h i v y o n i k awa naugua kifua mara kwa mara na ilinichukua muda mrefu kuzoea mazingira na kuanza kufanya vizuri.
UNADHANI UNAWEZA KUWA MFUNGAJI BORA MSIMU HUU?
“Licha ya ushindani kuwepo kwenye ligi na mimi nikiwa nimefunga mabao matano sijakata tamaa bado ninaamini kuwa naweza kumpindua Emmanuel Okwi pale alipo sasa na nikawa mfungaji bora sababu lolote linaweza kutokea.
“Bado tuna mechi nane mkononi, huwezi jua mechi ijayo naweza kupiga ‘hat trick’ au nikafunga hata mabao manne, hilo linawezekana na nikiweka juhudi naweza kuwa mfungaji bora msimu huu.
VIPI USHINDI KWENYE LIGI?
“Ushindani umekuwa mkubwa kwa sasa katika ligi jambo ambalo limekuwa mtihani kwa timu nyingi sababu ukiteleza mechi moja basi unashuka na ukishinda tu unapanda hasa kipindi hiki cha lala salama.
MALENGO YAKO NI YAPI?
“Kwanza kuhakikisha nafanya vyema msimu huu kwa kutimiza malengo yangu na ya klabu kama ambavyo tumejiwekea kuhakikisha tunamaliza tukiwa katika tano bora, hivyo tunapambana kutoka pale kwenye nafasi ile ya saba mpaka kuingia nafasi tatu za juu.
KWA NINI UNAPENDA KUVAA JEZI NAMBA 10?
“Hii kwangu ni kama namba yenye bahati kwangu ndiyo maana nilivaa nilipokuwa Stand na sasa hapa naendelea kuitumia.
BEKI GANI ANAYEKUSUMBUA UWANJANI?
“Beki ambaye ananipa mawazo hasa ninapokaribia kukutana naye ni Aggrey Moris wa Azam FC amekuwa akinitesa sana kuliko mabeki wengine hata (Kelvin) Yondani mwenye hamfikii Moris, yuko vizuri siyo rahisi kukabiliana naye na kumshinda.
MASHABIKI WATEGEMEE NINI KUTOKA KWAKO?
“Wategemee mazuri tu lakini kikubwa ni kuendelea kutupa sapoti na wasichoke naamini msimu huu tutamaliza vizuri licha ya ushindani kuwa mkubwa,” anasema Salamba.
Comments are closed.