The House of Favourite Newspapers

Simba SC Watenga Mechi Tano

KWA mujibu wa benchi la ufundi la Simba, wametenga mechi 5 ambazo zimebeba pointi zitakazowapa ubingwa. Simba ya Mfaransa Pierre Lechantre kwa sasa ndiyo inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 46, sawa na Yanga ambao nao wana idadi hiyo ya pointi.

 

Kikosi hicho katika michezo hiyo 10 yenye pointi 30 mechi tano watazichezea katika Uwanja wa Taifa huku tano wakizicheza mikoani.

Mechi ambazo Simba watafuata pointi mkoani ni pamoja na Majimaji ya Songea, Lipuli FC ya Iringa, Singida United ya Singida, Njombe Mji ya Njombe na Mtibwa Sugar ya Morogoro.

 

Kocha msaidizi wa kikosi hicho, Masoud Djuma raia wa Burundi amesema; “Tunatakiwa kuweka malengo ya kupata pointi kwenye mechi zote za mikoani.”

 

Kama Simba watafanikiwa kupata ushindi katika michezo yote hiyo watavuna pointi 30 ambazo ukijumlisha na 46 ambazo wanazo sasa watafikisha pointi 76 zitakazokua 3 mbele ya Yanga watakaomaliza ligi wakiwa na 73.

Comments are closed.