The House of Favourite Newspapers

Ruvu Shooting Yajiandaa ‘Kuipapasa’ Yanga

Kikosi cha Ruvu Shooting

BAADA ya Ruvu Shooting kufanikiwa kukusanya pointi nane katika mechi nne mfululizo, timu hiyo imesema kazi yake sasa ni kutoa dozi tu kwa mtindo wa kupapasa bila ya kuangalia wanakutana na nani hata Yanga.

 

Ruvu Shooting ambayo kwa sasa inashika nafasi ya saba ikiwa na pointi 32, mara ya mwisho kupoteza mchezo kwenye ligi ilikuwa ni Machi 3, mwaka huu ilipofungwa na Njombe Mji mabao 2-1.

 

Baada ya hapo, matokeo ya mechi zao yamekuwa hivi; Ruvu Shooting 2-2 Mbeya City, Ruvu Shooting 0-0 Prisons, Ruvu Shooting 2-0 Azam na Ndanda 1-3 Ruvu Shooting.

 

Akizungumzia hilo, ofisa habari wa timu hiyo, Masau Bwire, alisema: “Hivi sasa Ruvu Shooting ni moto wa kuotea mbali, hao waliosalia ambao bado hatujacheza nao wakiwemo Yanga wajipange na wajiweke tayari kupapaswa.”

Ikumbukwe kuwa, Yanga na Ruvu Shooting zinatarajiwa kupambana Mei 20, mwaka huu ikiwa ni mchezo mmoja kabla ya kumalizika kwa msimu huu.

Stori: Omary Mdose, Championi Jumatano

Comments are closed.