The House of Favourite Newspapers

Ukinunua Spoti Xtra Kesho Unashinda Jezi

GAZETI makini la michezo na burudani kila Jumapili la Spoti Xtra, kesho litatoa zawadi orijino kwa wasomaji wanne.

 

Spoti Xtra ambalo limetokea kukubalika na wasomaji kwa muda mfupi kutokana na chambuzi na habari zake za kitaifa na kimataifa, litatoa zawadi za jezi orijino za Ligi Kuu England na Headphones za Beats by Dre kutoka Marekani.

 

Ni rahisi kabisa. Wasomaji watajishindia zawadi hizo kupitia shindano linaloendelea kwenye gazeti hilo ambapo watatakiwa kununua nakala na kutuma namba iliyopo kwenye ukurasa wa pili kadri msomaji anavyotaka.

Droo ya shindano la kesho Jumapili itachezeshwa laivu Alhamisi ijayo saa 10:00 jioni kupitia Kipindi cha Spoti Hausi cha Global Tv Online na mshindi atapewa utaratibu wa kuchukua zawadi yake.

 

Waliojishindia kwenye shindano la wiki iliyopita ni Fadhil Ramadhani mkazi wa Mkuranga aliyejipatia zawadi ya Headphones orijino za Beats by Dr Dre huku Mkazi wa Vingunguti, Juma Saleh akijishindia jezi ya Everton.

 

Godluck Mushi ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) naye alishinda jezi ya Arsenal pamoja na Ally Bobea wa Kibaha aliyejinyakulia uzi wa Manchester City.

 

Baadhi ya washindi hao watakabidhiwa zawadi zao keshokutwa Jumatatu Jijini Dar es Salaam kwenye ofisi za Spoti Xtra zilizopo Sinza, Mori.

Comments are closed.