The House of Favourite Newspapers

Lechantre Ajaa Kiburi Mechi Ya Yanga SC

Pierre Lechantre akifanya yake.

KOCHA wa Simba, Pierre Lechantre ameanza kiburi kuelekea mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga kwa kuse­ma amefurahi uwepo wa kiungo wake mkabaji, Jonas Mkude katika mchezo huo.

 

Mkude hakucheza mechi iliyopita ya Simba wikiendi iliyopita dhidi ya Lipuli FC kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa iliyoisha kwa sare ya bao 1-1. Mkude alikuwa akitumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Lechantre alisema anafurahi uwepo wa Mkude katika mechi hiyo dhidi ya Yanga ambayo ni ngumu ili kuhakikisha anapata ush­indi na kubaki kileleni mwa ligi hiyo.

Lechantre alisema, katika mechi iliyopita timu yake ilizidiwa katika safu ya kiungo baada ya kumkosa Mkude, hivyo hana hofu katika mch­ezo wa marudiano dhidi ya Yanga kwani tatizo hilo halitaonekana.

 

“Katika timu unapomkosa mche­zaji muhimu anayeendana na mfumo wako inakuwa ni ngumu timu kucheza vile ninavyotaka kama ilivyo­jitokeza katika mechi na Lipuli.

 

“Alikosekana Mkude ambaye ndiye injini ya timu anayecheza kwa kuu­fuata mfumo na maelekezo yangu na kusababisha kupata matokeo mabaya ya sare.

 

“Mkude anacheza vizuri na kufuata maelekezo yangu na niseme ninafura­hia kiwango kikubwa anachoendelea kukionyesha katika mechi za ligi am­bazo zinaendelea,” alisema Lechantre.

Simba kwa sasa ipo kambini Morogoro kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa Jumapili wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

Comments are closed.