The House of Favourite Newspapers

TTCL PESA YABADILI JINA NA NEMBO

Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL), imebadili nembo na jina la iliyokuwa TTCL Pesa na sasa kujulikana kama T Pesa baada ya Uzinduzi uliofanyika jijini Dodoma leo.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL CORPORATION), Waziri Kindamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa Nembo ya na jina lipya la TTCL Pesa.
Meza Kuu ikifuatilia matukio wakati wa uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTCL Corp, Omar Nundu akizungumza.
Mgeni Rasmi, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasilaino (Sekta ya Mawasiliano), Atashasta Nditiye akizungumza wakati wa usimduzi huo.

TTCL PESA, Kampuni tanzu ya Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Corporation, ambao ni watoaji
wa huduma za fedha mtandao inapenda kuwajulisha Wateja, Wadau na Umma kwa ujumla kwamba,
imefanya mabadiliko ya Jina na Nembo zinazoitambulisha Kampuni hiyo.

TTCL PESA ilizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Mama Samia Suluhu Hassan tarehe 18 Julai 2017 ikiwa na lengo kuu la kuwapa Wananchi huduma za kiwango cha juu kabisa cha ubora na unafuu  wa gharama za kutuma fedha, kupokea fedha, kulipia huduma na kufanya miamala mbalimbali kwa kutumia simu zao.

Mabadiliko haya yanakuja miezi 9 baada ya TTCL PESA kuanza huduma zake kwa Mafanikio
makubwa.

Hatua hii ni kuridhia ushauri wa Wateja na wadau wetu waliopendekeza kufanyika
mabadiliko ya jina na Nembo ili kuongeza mvuto wa huduma, kukidhi mahitaji ya Soko na urahisi wa
kuitambua huduma hii miongoni mwa huduma zinazotolewa na Taasisi nyingine.
Huduma za fedha Mtandao ni Sekta inayokua kwa kasi duniani kote.

 

Hapa Nchini Tanzania, miamala inafanyika katika jamii kupitia njia hii na kusaidia sana katika kuokoa muda, kurahisisha manunuzi, kutoa ajira kwa Makundi mengi ya wananchi hasa Wanawake na Vijana, kuongeza Mapato ya Nchi kupitia tozo za kodi, kuongeza usalama wa fedha na kuepusha uwezekano wa vitendo vya kihalifu
kama wizi na utapeli visiweze kutokea kwa urahisi.

Kwa kutambua umuhimu wa Jina la huduma na Nembo kuwa ni nyenzo muhimu sana katika mikakati
ya Biashara na hasa biashara yenye ushindani mkubwa kama hii ya Fedha Mtandao, TTCL
Corporation inaamini kuwa, Jina na Nembo mpya zitakidhi mahitaji ya Wadau na Ushindani wa soko
sambamba na kusaidia harakati za kuongeza kasi ya kusambaa kwa huduma za Fedha Mtandao
zinazotolewa na Shirika letu kupitia Kampuni yake tanzu ya TTCL PESA.

Tunaileta T-Pesa kuja kuwa muhimili mkuu wa miamala ya kifedha Tanzania. Tunamlenga kila
mwananchi kufaidika na huduma za tpesa ambazo zimekuwa nafuu na salama zaidi. Uzinduzi wa
nembo hii ni mwanzo wa mambo mazuri na makubwa yatakayoletwa na T-Pesa.

 

Nia yetu ni kuwa sehemu ya kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi kwa kuhakikisha tunatoa suluhisho la uhakika
katika miamala ya kifedha hususani katika malipo ya huduma za umma and ukusanyaji wa malipo hayo.

 

T-Pesa itashirikiana na taasisi zote za umma, mabenki na taasisi binafsi katika kufikia malengo
haya na mwisho kutoa huduma bora nafuu na za uhakika kwa watanzania.
Imetolewa na;
Ofisi ya Uhusiano,
TTCL Makao Makuu,
Dar Es Salaam.
3 Machi, 2018

(Picha:Mroki Mroki-Daily News Digital)

Comments are closed.