The House of Favourite Newspapers

Nunua Spoti Xtra Kesho Jumapili Upate Jezi Orijino

WASOMAJI wa Gazeti la Spoti Xtra kesho Jumapili, mbali na kupata uhondo wa aina yake kwenye habari, makala na chambuzi mbalimbali watafaidi zawadi za kumwaga ambazo ni orijino kutoka Ulaya.

 

Spoti Xtra ambalo kesho litakuwa na Toleo Maalum la El Clasico, litatoa zawadi kwa wasomaji wake kupitia shindano lililopo kwenye gazeti hilo kama sehemu ya shukrani kwa kukubalika kwa haraka sokoni na kuyazidi kete magazeti makongwe.

 

Kwa mujibu wa Mhariri wa Spoti Xtra, Michael Momburi ni kwamba, kila msomaji atakaponunua gazeti kwenye ukurasa wa pili kuna kuponi ya jinsi ya kushiriki na akishatuma namba atakuwa ameingia moja kwa moja kwenye droo itakayochezwa Alhamisi.

 

Zawadi zinazoshindaniwa ni headphones orijino za Beats by Dre kutoka Marekani pamoja na jezi za klabu za Ligi Kuu ya England ambako kila mshindi atapewa jezi ya klabu atakayochagua.

 

Spoti Xtra litatoa jezi tatu kwa wasomaji wake watakaoshiriki shindano la kesho Jumapili na droo itachezwa kwenye kipindi cha Spoti Hausi kinachorushwa na Kituo cha Global TV Online kila Alhamisi saa 10:00 jioni.

 

Washindi watapigiwa simu moja kwa moja na kuambiwa zawadi walizoshinda na siku inayofuata watakabidhiwa kwenye Ofisi za Spoti Xtra zilizopo Sinza Mori, Dar es Salaam.

 

Kumbuka, Spoti Xtra linauzwa kwa Sh 500 tu na linasomwa na mashabiki wote makini wa michezo nchini Tanzania kwa sasa kila Jumapili.

Comments are closed.