The House of Favourite Newspapers

WOLPER AMKABIDHI HARMONIZE KWA MUNGU

KWELI hii inaitwa chuki nichukie, lakini moyo wangu niachie! Hivi ndivyo ilivyo sasa kati ya staa wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper Massawe kuamua kutoa la moyoni baada ya mpenzi wake wa zamani, Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ kumuanikia msururu wa wanaume aliotembea nao.

 

Wolper ambaye wikiendi iliyopita alikuwa akirushiana maneno makali na Harmonize aliiambia Over Ze Weekend kuwa, kwa sasa ameamua kunyamaza na badala yake amemkabidhi jamaa huyo kwa Mungu kwani hatamjibu chochote endapo ataendelea kumdhalilisha mitandaoni.

 

“Sitaki kabisa kuendelea kubishana naye, ameamua kunidhalilisha, lakini mimi namuachia Mungu, ndiye atamjibu,” alisema Wolper.

 

Wolper na Hamornize walianza kurushiana maneno makali baada ya Wolper kuandika kuwa mpenzi mpya wa mwanamuziki huyo, Sarah, ni mlezi wa wana, jambo ambalo lilimtibua Harmonize ambaye naye alijibu mapigo kwa kumhorodheshea wanaume aliotembea nao.

IMELDA MTEMA

EXCLUSIVE: Harmonize Kajibu, Mwarabu Kutembea na Sarah Wake

 

Comments are closed.