NIWAPONGEZE Simba ambao kwa msimu huu wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kuonyesha juhudi ya hali ya juu tangu kuanza kwa ligi, lakini pongezi zangu za dhati ziende kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na kufanikiwa kwa kiasi fulani katika usimamizi wa ligi zetu za ndani.
Licha ya misuguano na changamoto za hapa na pale ambazo ni ngumu wakati mwingine kuziepuka kutokana na miundombinu ya nchi yetu ingawa naamini huu ni mwanzo tu wa kuelekea katika mabadiliko makubwa ya kimipango katika soka letu.
Lakini ukiondoa ubingwa wa Simba ambao bado wamebakiwa na mechi mbili za kukamilisha mechi 30 za Ligi Kuu Bara wakiwa sawa na Azam ambao wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 52 wakifutia na Yanga ambao wanakamata nafasi ya tatu na pointi zao 48 huku wakiwa na mechi nne mkononi.
Kwa sasa vita ya ubingwa imeshafikia ukingoni baada ya Simba kufanikiwa kutwaa wakiwa na pointi 68 isipokuwa vita kubwa ipo kwa upande wa Azam na Yanga katika kugombania nafasi ya pili ingawa Yanga wana nafasi kubwa ya kuweza kuichukua kutokana na idadi ya mechi waliobakiwanazo tofauti na Azam ambao wana mechi mbili pekee.
Naamini hapa lazima patachimbika kwa timu hizo kuhakikisha wanafanya vizuri katika mechi zilizobakia ili kuweza kupata nafasi hiyo ingawa haitaweza kusaidia kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao kwa kuwa mshiriki wake anatoka kwenye Kombe la FA.
Upande mwingine tumeweza kuishuhudia timu yetu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes ikishindwa kupata matokeo ya ushindi katika mchezo wake wa kuwania kufuzu fainali za vijana zitakazofanyika Niger baada ya kufungwa mabao 2-1 na Mali.
Matokeo hayo, binafsi naamini hayakustahili kupata timu yetu ya vijana kwa kuwa walikuwa kwenye uwanja wa nyumbani lakini ndani yake ukiangalia kwa makini unaona timu yenyewe inakosa muunganiko wa kutosha licha ya mwalimu wake Ammy Ninje kuwa na maneno mengi lakini upande wa vitendo bado shida.
Ngorongoro hawakustahili kufungwa na Mali kwa kuwa Mali hawa ndiyo ilikutana na Serengeti Boys katika michuano ya vijana kule Gabon na hata kama kuna mabadiliko yaliofanyika basi yalikuwa machache kwa upande wa Mali na Ngorongoro k w a n i w a c h e z a j i wao walip a n d i s hwa madaraja.
L a k i n i k u t o k a n a na mipango mibaya ya m w a l i m u , timu ilishindwa kupata ushindi ingawa tunaweza kwenda kufanya vizuri kwao iwapo benchi la ufundi litafanya maamuzi sahihi.
Nikiachana na hayo, leo Jumatano wawakilishi wa Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga, watacheza mechi yao ya pili katika Kundi D, dhidi ya Rayon Sport kutoka nchini Rwanda huku ikiwa imeshapoteza mchezo wa kwanza dhidi ya USM Alger.
Katika mchezo huo utakaopigwa saa moja usiku kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, Yanga inapaswa kupambana na kuhakikisha inapata ushindi ili kuweza kujiwekea mazingira mazuri kwa kuwa ukiangalia mpaka sasa hakuna timu ambayo ina nafasi kwenda hatua ya robo fainali ikiwemo Gor Mahia kutoka kundi hilo.
Kweli hakuna asiyejua kwamba Yanga ipo katika hali mbaya ya kiuchumi lakini hii isiwe sababu ya wao kushindwa kufanya vizuri kwa kuwa ushindi watakaoweza kupata leo ndiyo pesa yenyewe itakayoweza kuwalipa wao.
Niwaambie wachezaji haya masuala ya timu kukosa fedha za kulipa wachezaji hata wakati wetu yalikuwepo lakini kikubwa wachezaji tulikuwa tukiangalia na maslahi ya timu zetu, yaani nini inachokihitaji ili kuweza kufikia malengo na kwa nini wakati wenu liwe tatizo ambalo wengine linasababisha kugomea kucheza.
Binafsi naona huu ndiyo wakati wa wachezaji kuungana kwa kupata ushindi wakati masuala yenu yanafanyiwa kazi kwa kuhakikisha Rayon anafungwa kwenye Uwanja wa Taifa kwa kuwa ukubwa na thamani ya mashindano haya ni kuwa na sehemu ya kuweza kujiuza kama mchezaji na siyo kufanya michezo ya kugomea.
UCHAMBUZI: Mohammed Hussein
Comments are closed.