22 Wafariki, Zaidi ya 22 Wajeruhiwa Katika Mlipuko China

MLIPUKO kwenye kiwanda cha madawa jijini Zhangjiakou, katika jimbo la Hebei, kaskazini mwa China, mapema leo, umeua watu 22 na zaidi ya 22 kujeruhiwa. 

Mlipuko huo ulioibua moto na moshi mkubwa, uliteketeza pia magari 50 na kusababisha viwanda vya jirani kufungwa.

Vyombo vya habari vya serikali vilisema moto uliozuka Zhangjiakou, jiji lililo umbali wa kilomita 156 kaskazini-magharibi mwa Beijing, umezimwa.  Mji huo na Beijing unatazamiwa kuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi mwaka  2022.


Mnamo August  2015, watu 165 waliuawa baada ya mlipuko uliotokea katika ghala la madawa jijini Tianjin kutokana na kuhifadhiwa ovyo kwa madawa hayo.

 

Toa comment