The House of Favourite Newspapers

KIONGOZI, ZANZIBAR STARS ATAABIKA NA FIGO

Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Utalii nchini, Rashidi Shabani

KIONGOZI wa Kundi la Zanzibar Stars Modern Taarab na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Utalii nchini, Rashidi Shabani maarufu Rashidi Mukubwa, yuko katika wakati mgumu kufuatia kusumbuliwa na tatizo la figo na kumfanya muda mwingi awe kitandani na kushindwa kufanya shughuli zake za kimaisha.

Rashidi Mukubwa ambaye wakati mwingine alikuwa akiitwa jina la Bonge kutokana na ukubwa wa umbo la mwili wake, tatizo la figo limemfanya apoteze hamu ya kula na kupungua uzito na umbo lake.

Akizungumza na mwandishi wetu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar hivi karibuni ambapo alikwenda kusafishwa figo zake ambazo zote zimeshindwa kufanya kazi na hivyo kuishi kwa msaada wa mashine maalum, alisema anaomba habari hizi ziwafikie wadau mbalimbali ili waweze kumsaidia kupambana na gharama za matibabu ambazo nazo zimeanza kumuelemea kutokana kushindwa kufanya kazi ya kuingiza kipato tangu alipoanza kusumbuliwa na tatizo hili lililobainika mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu.

Rashidi amesema madaktari wanaomtibu katika hospitali hiyo wamemuambia kuwa gharama ya kubadilisha figo hizo ni shilingi milioni thelathini. Kutokana na kushindwa kumudu kiwango hicho cha pesa amekuwa akitumia huduma ya kusafishwa figo hizo kwa gharama ya shilingi laki moja ambapo kwa wiki anatakiwa kusafishwa mara mbili wakati akisubiri kupata pesa ya kubadilisha figo hizo.

Kwa Msamaria Mwema anayetaka kumjulia hali au kupata maelezo yoyote ampigie mwenyewe kwenye simu yake namba 0784-288678.

Habari na Richard Bukos

 

Comments are closed.