Taarifa Maalum Kwa Wasomaji Wa Magazeti Ya Global Publishers

Uongozi wa Global Publishers Limited, wachapishaji wa Magazeti ya Uwazi, Championi, Ijumaa, Risasi, Amani, Ijumaa Wikienda na Spoti Xtra, unapenda kuwatangazia wasomaji wake nchi nzima kuwa, kuanzia Juni 15, 2018 bei ya magazeti yetu ya shilingi 500 itabadilika na kuwa shilingi 800.

 

Tumelazimika kufanya mabadiliko hayo ya bei kutokana na kupanda kwa gharama za uchapishaji
na usambazaji ambazo zimeongezeka kwa kiasi kikubwa.

 

Pamoja na mabadiliko hayo ya bei, tumefanya mabadiliko makubwa katika uandishi wa habari za michezo, burudani, matukio ya wasanii, kijamii na kiuchunguzi na tunawaahidi wasomaji wetu kuendelea kuwapa habari za kipekee na za uhakika.

 

Usikose kufuatilia magazeti yetu kwani kutakuwa na zawadi kabambe zitakazotolewa kwenye magazeti hayo kila siku!

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment