The House of Favourite Newspapers

Simba, Yanga Zilienda Kiujanja-Ujanja Kenya, Zimestahili Zilichokipata

Kikosi cha timu ya Simba.

 

PONGEZI zangu za dhati ziende kwa mwekezaji wa Simba, Mohamed Dewji ‘Mo’ kwa kile ambacho alikifanya juzi Jumatatu kwa kutoa tuzo kwa wachezaji na watu mbalimbali wa timu hiyo. Ni jambo ambalo linaamsha hamasa kwa kila mchezaji kwa ajili ya kupam­bana kuitumikia timu.

 

Niwapongeze wote ambao wamepata tuzo na hata wale ambao hawajapata basi ni wazi kwamba nao wajitoe ili siku ny­ingine nao waweze kupata fur­sa kama hiyo ya kutwaa tuzo. Pia kwa klabu nyingine kufanya kitu kama hicho siyo dhambi kwani kinaongeza upambanaji kutoka kwa mchezaji mmoja kwenda mwingine.

 

Baada ya hayo, sasa acha niende moja kwa moja kwenye mada yangu husika; wikiendi iliyopita michuano ya SportPe­sa Super Cup ilihitimishwa kule Kenya. Ikumbukwe kwamba kampuni ya SportPesa ndiyo wadhamini wa klabu zetu za Simba, Yanga, Singida United na JKU kutoka visiwani Zanzi­bar.

 

Mwisho wa fainali hiyo am­bayo kwa upande wetu Tanza­nia tuliwakilishwa na Simba, ilimalizika kwa kikosi hicho kuchapwa mabao 2-0. Mabao hayo walifungwa siyo kwa ku­bahatishwa bali yalitokana ka­bisa na uwezo wao waliouonye­sha kwenye mchezo huo.

Kikosi cha timu ya Yanga.

Licha ya kukosa kitita cha milioni 68 lakini wamekosa na­fasi ya kwenda nchini England kucheza na Everton na ku­waruhusu kwa mara nyingine tena Gor Mahia kucheza na timu hiyo kama walivyofanya mwaka jana kwenye ardhi yetu jijini Dar.

 

Kwangu mimi naona kabisa timu zetu zimevuna kile am­bacho walikipanda kabla ya kuanza kwa tuzo hizi; ukitazama jinsi wawakilishi wetu namna walivyoondoka hapa nchini uta­baini kabisa kwamba walienda kimasihara na kutoyapa kabisa uzito mashindano haya am­bayo kama yangetumika vizuri, nadhani ingekuwa fursa nzuri kwa wachezaji wetu kutoka kisoka.

 

Wawakilishi wote wanne, Simba, Yan­ga, Singida United na JKU walikuwa na maandalizi ya kulipua kabla ya kwenda Kenya am­bapo waliku­tana na wenzao ambao wanajua umuhimu wa mashindano hayo na mwisho ndiyo tumejikuta tukiambulia nafasi ya pili na tatu huku tukii­acha kabisa nafasi ya kwenda England kucheza na Everton.

 

Nasema maandalizi ya kuli­pua ni kutokana na aina ya matokeo ambayo timu zetu ziliyapata tangu kuanza kwa mashindano hadi pale yanapoi­sha. Katika dakika zote ambapo wawakilishi wetu walishuka dimbani hakuna hata timu moja ambayo ilionja utamu wa ush­indi katika daki­ka 90 zaidi ya kusubiri faraja ya penalti kwa ajili ya kuwavu­sha na kuingia hatua zinazoku­ja.

 

Nitoe rai kwamba tu­natakiwa ku­badilika hasa pale inapokuja michuano ya namna hiyo kwa kuhakikisha kwamba tuna­jiandaa kikamilifu kwa ajili ya kushindana na siyo kushiriki kama walivyofanya walioenda Kenya kuona kwamba licha ya kutwaa kombe lakini tunapata fursa kama hizo za kwenda kucheza nje ya nchi.

 

Niwapongeze Gor Mahia kwa umakini ambao waliounyesha tangu walipoanza kucheza mechi yao ya kwanza na wa­likuwa wanajua nini ambacho wanakitafuta ndani na nje ya uwanja na ndiyo maana mwisho wakafanikiwa kutwaa ubingwa.

 

Kucheza ndai ya Goodson Park ambao ni Uwanja wa Ever­ton kutawapa nafasi wachezaji wa Gor Mahia kuonekana na mawakala wa kimataifa ambao wataweza kuwachukua na ku­wapeleka hata katika ligi za ma­daraja ya chini sitarajii kuona kikosi hicho kikienda England na kurudi bila ya faida yoyote.

 

Nafasi hiyo ilitakiwa iwe kwa nyota wetu wa hapa nchini la­kini imeshindikana kwa sababu tu hawakutulia maanani kombe kama hilo na kupeleka timu ambazo ni dhaifu kuliko wap­inzani wao, kitendo kama hicho tusikirudie tena pale itakapo­tokea michuano kama hiyo.

Makala na Mohammed Hussein

Comments are closed.