The House of Favourite Newspapers

Breaking: Diamond Anusurika Ajalini Marekani

 

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz,  amenusurika katika ajali ya gari nchini Marekani ambako anatangaza albamu yake ya ‘A Boy From Tandale’. Muimbaji huyo amepata ajali hiyo wakati akitokea kwenye shoo huko California.

 

Kupitia mtandao wa Instagram ameandika:

Dah Tumepata ajali na kunusurika kufa usiku wa leo wakati tunatoka kwenye show….ila Mwenyez Mungu ametupa nafasi nyingine tena ya kuishi na kuendelea kushikana mkono na vijana wenzangu mtaani kwa pamoja tuziokoe familia zetu duni🙏🏻….

Diamond ndiye mwanzilishi na mmiliki wa lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) ambayo inasimamia wasanii kama Harmonize, Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen, Lava Lava na Mbosso.

Ajali hiyo ilimkuta akiwa na wenzake ambao ni pamoja na DJ wake,  Rommy.

Comments are closed.