Richard Tanganyika Akabidhiwa Pikipiki ya ‘Tusua Maisha na Global’





MSHINDI wa pikipiki katika Shindano la Tusua Maisha na Global, Richard Tanganyika, amekabidhiwa zawadi yake pamoja na washindi wengine katika ofisi za Global Group, zilizoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
Washindi wengine waliokabidhiwa zawadi zao ni Shaaban Kamoye aliyejishindia dinner set, Nasoro Juma aliyejishindia headphones za kisasa, za Beats by Dre na Novart Magere aliyejishindia jezi, ambaye amewakilishwa na ndugu yake, Hassan Mathias.
Kushinda ni rahisi, nunua gazeti lolote la #GlobalPublishers la #Uwazi, #Amani, #Ijumaa, #IjumaaWikienda, #RisasiMchanganyiko, #RisasiJumamosi, #Championi, #SpotiXtra kisha fuata maelekezo ukurasa wa pili.
(PICHA: RICHARD BUKOS | GPL)


Comments are closed.