The House of Favourite Newspapers

SINGIDA YAMSHTUA KAGERE ATAKIWA KUJIONGEZA

Meddie Kagere.

MEDDIE Kagere ambaye mashabiki wa Gormahia wakisikia jina lake wanashtuka, ameangalia kiwango cha Singida United akasisitiza kwamba anahitaji kujiongeza msimu ujao ndani ya kikosi cha Simba.

 

Kagere ambaye alipewa uraia wa Rwanda hivi karibuni akiwa mzaliwa wa Uganda, anasema; “Singida kwangu bado ni timu nzuri na inanipa changamoto mpya ya kuweza kujipanga ili nione nawezaje kufanikiwa katika ligi haijalishi kitu gani nimekifanya nyuma ndiyo maana nasema lazima nijipange ili niweze kuendana na kasi ya ligi ya hapa.

 

“Kikubwa ambacho nakiona kwa upande wangu hii ni moja kati ya timu ambazo nitakutana nazo kwenye ligi, uchezaji wao umenipa kitu ninachopaswa kukifanya kiwe bora na kuweza kuendana na kasi ya ligi kutokana na nilivyowaona katika mechi mbili ambazo nilicheza dhidi yao,” alisema Kagere ambaye ameondoka Gormahia bure walipokuwa wakijishauri kumpa mkataba mpya.

STORI: IBRAHIM MUSSA, SPOTI XTRA

Comments are closed.