The House of Favourite Newspapers

Jose Mourinho Vs Man United

Jose Mourinho

KWA kawaida mako­cha na wachezaji wen­gi huwa wanatumia mechi za maandalizi ya msimu kwa ajili ya kuwa kitu kimoja, kufundishana mbinu na hata mechi zinazo­chezwa hapo huwa siyo zile za kutumia nguvu.

Ikiwa imesalia wiki moja kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’, upande wa Man­chester United hali ni tofauti, kwa ufupi ni kama upepo umevurugika klabuni hapo.

 

Mhusika mkuu katika ‘kivuruge’ hicho ni kocha wa timu hiyo, Jose Mourinho ambaye amekuwa aki­toa lawama kadhaa juu ya baadhi ya mambo kutokwenda sawa.

 

United iliamua kwenda Mareka­ni kufanya ziara hiyo ya kujiandaa na msimu, lakini inavyoonyesha wazi Mourinho hana uhusiano mzuri na bosi wake, Ed Woodward ambaye ni makamu mwenyekiti kuhusu sera ya usajili.

 

Mourinho ameweka wazi kuto­furahishwa na usajili uliofan­yika, alinukuliwa akisema alitoa mapendekezo yake ya wachezaji anaowahitaji na anahisi hatawa­pata wote anaowahitaji.

Wakati dirisha la usajili likitara­jiwa kufungwa usiku wa Alhamisi ijayo Agosti 9, Mourinho amekuwa akiwatolea kauli kali wachezaji wake hadharani kiasi cha kuamini­ka kuwa hawana furaha na aina ya ukosoaji wake huo.

 

Baadhi ya mambo ambayo amekuwa akilalamika ni ratiba ya mechi za kirafiki kuwabana, wache­zaji wake kutokuwa fiti, kukosa wachezaji wa kikosi cha kwanza na kuwalaumu viongozi wake kwa kutotimiza usajili anaohitaji.

 

Huu ni uchambuzi wa kukum­busha wachezaji wa United am­bao wametolewa kauli tata kutoka kwa Mourinho ambaye alimaliza msimu uliopita akiwa hana taji lol­ote.

 

MOURINHO VS ANTONIO VA­LENCIA

Hii imewashangaza wengi kwa kuwa mkongwe huyu hana kawa­ida ya kukwaruzana na makocha wake tangu aanze kucheza soka la kulipwa.

Alimkosoa beki wake wa kulia, Valencia kuwa hakuwa fiti, alirejea kutoka likizo akiwa hana mazoezi na ndiyo maana akaumia kirahisi.

“Nafikiri Antonio Valencia alikuwa na likizo ndefu kwake, hakuwa na hali nzuri, baada ya muda akau­mia,” alisema Mourinho baada ya United kuchapwa 4-1 na Liverpool.

Kuumia kiazi cha mguu kwa Va­lencia kutamfanya kukosa mechi ya ufunguzi wa Premier League dhidi ya Leicester City.

MOURINHO VS ANTHONY MARTIAL

Msimu uliopita alikuwa akimpa nafasi mara kad­haa, alipoona hajafikisha ubora anaouhitaji akaanza kumpiga benchi, hivi karibu­ni uhusiano wao unaoneka­na kuzidi kulegalega.

Martial aliondoka kambiini kurejea Ufaransa ambako mpenzi wake aliji­fungua, Mourinho hakufurahia hilo na akanukuliwa akisema kuwa hakutoa baraka za safari hiyo.

Mbali na hapo Mourinho amekuwa akimkosoa mara kadhaa Mfaran­sa huyo kiasi cha kumfanya aanze kutafuta mlango wa kutokea.

“Anthony Martial amejaaliwa kupa­ta mtoto, baada ya kuhakikisha ana afya njema alitakiwa kumshukuru Mungu na kurejea kazini, lakini hadi sasa hajarudi na sijui kwa nini,” al­isema Mourinho.

 

MOURINHO VS CHRIS SMALL­ING/PHIL JONES

Msimu wa 2016-17, Mourinho aliwa­kosoa walinzi wake hao wa kati kwa kuwa na sababu nyingi za kutofan­ya vizuri. Hata walipoumia walikaa muda mrefu nje jambo ambalo lilim­kera kocha huyo.

 

MOURINHO VS LUKE SHAW

Mchezaji ambaye ameongoza kwa kukosolewa na Mreno huyo ni Shaw ambaye ni beki wa kushoto, ame­kuwa akisemwa na kocha huyo kuwa ni mzito, hajitumi, mgumu kuelewa na mambo mengine kama hayo.

Mourinho amekuwa hafichi hisia zake kwa kumkosoa mchezaji huyo hadharani. Mbali na hapo aliwahi kulalamika kuwa akiumia kidogo anashindwa kucheza na kuomba udhuru.

Kuna wakati alitoa kauli hii: “Ni vigumu kumuweka Shaw hata benchi tu kwa kuwa siwezi kumfa­nanisha na Ashley Young, (Mat­teo) Darmian na (Daley) Blind.”

 

MOURINHO VS HENRIKH MKHI­TARYAN

Mourinho ndiye ambaye alimsajili lakini baadaye alioona anashindwa ku­fanya kile anachotaka, ikabidii amuuze kwenda Arsenal.

“Sikufurahishwa na kiwango chake, sizungumzii mechi moja au mbili bali ni nne au tano, alianza msimu vizuri lakini baada ya muda akawa anarudi nyuma katika ufungaji na hata kutoa asisti, hakuwa vizuri katika majukumu yake ya namba kumi,” alinukuliwa Mourinho.

 

MOURINHO VS PAUL POGBA

Hapa ndipo shughuli ipo, Mourinho alimsajili kwa pauni 89m na kuweka rekodi wakati huo ya kuwa mchezaji ghali zaidi kusajiliwa duniani.

Baada ya kutwaa ubingwa wa dunia, wengi walitegemea Mourinho atamsi­fia staa wake huyo lakini kauli alizotoa kuhusu Pogba zilionyesha wazi kuna mambo hayako sawa.

Msimu uliopita alimkosoa mara kad­haa Pogba hadharani kiasi cha kuamua kumpiga benchi katika mechi kadhaa.

 

MOURINHO VS MARCUS RASH­FORD

Mwishoni mwa msimu uliopita baada ya United kufungwa bao 1-0 na Brighton, Mourinho hakufura­hishwa na kiwango cha Rashford ambaye alipewa majukumu ya kush­ambulia lakini akajikuta akikosa na­fasi nyingi za wazi.

“Kwa nini Lukaku kila siku? Naamini mmeona sababu, wanashindwa kuonyesha uwezo binafsi, wachezaji wanaopewa nafasi badala ya wen­gine wanashindwa kuonyesha ukali wao na hawapo ka­tika levo inayotaki­wa,” alisema Mour­inho akimlenga Rashford.

Comments are closed.