The House of Favourite Newspapers

Abdi Kassim, Wema Sepetu Kumuaga Cannavaro Yanga

Wema Sepetu.

KIUNGO wa zamani wa Yanga, Abdi Kassim ‘Babi’ amefunguka kuwa amefurahia kitendo cha timu yake ya zamani cha kuandaa mchezo wa kumuaga aliyekuwa nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro.’

 

Cannavaro amestaafu kuichezea timu hiyo na sasa amepewa kazi ya umeneja kwenye kikosi hicho.

Babi ameyasema hayo kufuatia Yanga kuandaa mchezo wa kirafiki dhidi ya Mawenzi Market ya Morogoro ambayo anaichezea kiungo huyo utakaopigwa Agosti 12, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Nadir Haroub ‘Cannavaro.’

Babi ameliambia Championi Jumamosi kuwa: “Kwanza nawaambia mashabiki huu ni mchezo maalumu umewekwa kwa ajili ya Cannavaro kutoka uchezaji kwenda hatua ya umeneja wa timu na mambo ya uongozi kiujumla, kwa hiyo kwangu binafsi ninafurahi sana kukutana na Yanga maana mimi nitakuwa kwa upande wa Mawenzi Market na mechi itakuwa nzuri.”

 

Katika hatua nyingine, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa, kabla ya mchezo huo kutakuwa na burudani ya muziki kutoka kwa Mr Blue, Afande Sele, Lulu Diva, Juma Nature na Billnas huku Yanga Queens ambayo itaongozwa na Wema Sepetu itacheza na Morogoro Kombaini.

Comments are closed.