The House of Favourite Newspapers

Kipa Simba SC Apewa Adhabu Na Mbelgiji

WAKATI Simba leo ikicheza na Asante Kotoko ya Ghana katika mchezo wa kirafiki kwenye Tamasha la Simba Day, kocha mkuu wa timu hiyo, Patrick Asseums raia wa Ubelgiji, ameonekana ni mtu asiyependa utani awapo mazoezini.

 

Simba ambayo leo itacheza na As­ante Kotoko kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, juzi Jumatatu kikosi cha timu hiyo kilifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana, Dar, ambapo kocha huyo alimpa adhabu ya kupiga ‘pushapu’ kipa namba tatu wa kikosi hicho, Ally Salim kutokana na kushindwa kufuata maelekezo yake.

 

Katika mazoezi hayo ambayo yali­fanyika chini ya ulinzi mkali, Cham­pioni lilipata wasaa wa kuyashuhudia mwanzo mwisho.

 

Mbelgiji huyo alitoa adhabu hiyo wakati alipokuwa ametoa zoezi la kuonyoosha viungo ambapo kipa huyo hakufanya kama kocha alivyotaka hali iliyomfanya kupewa adhabu hiyo ya kupiga ‘pushapu’ tano.

Comments are closed.