MWILI WA MAJUTO UKITOKA NYUMBANI KWENDA MSIKITINI (PICHA +VIDEO)

MWILI  wa aliyekuwa msanii gwiji wa filamu nchini, Amri Athumani ‘King Majuto’,  unatarajiwa kuzikwa leo mkoani Tanga katika shamba lake lililopo katika kijiji cha Kiruku ambako maeneo ya Donge ambako viongozi mbalimbali wa serikali,  akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela, wamefika kushiriki maziko yake.

 

Mzee Majuto alifariki usiku wa Jumatano, Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Muhimbili, ambapo kesho yake, Agosti 9, 2018 mwili wake ulipelekwa katika Msikiti wa Maamur, Upanga, jijini Dar es Salaam, kuswaliwa kabla ya kupelekwa viwanja vya ukumbi wa Karimjee kuagwa. Baadaye mwili huo ulisafirishwa kuelekea jijini Tanga kwa maziko.

   

  PICHA: RICHARD BUKOS | GPL

Toa comment