The House of Favourite Newspapers

Ninja: Mtamsahau Cannavaro Wenu

BEKI wa kati wa Klabu ya Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’

BEKI wa kati wa Klabu ya Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’ amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo mara baada ya kukabidhiwa jezi namba 23 ambayo awali ilikuwa ikivaliwa na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwa kusema kuwa atapiga sana kazi.

 

Ninja alikabidhiwa jezi hiyo kwenye mchezo wa kumuaga Cannavaro ambao awali viongozi wa timu hiyo walitaka kuistaafisha isivaliwe tena kutokana na heshima ya beki huyo ambaye kaitumia jezi hiyo kwa muda mrefu.

Klabu ya Yanga Abdallah Shaibu ‘Ninja’.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Ninja amesema kuwa ana furaha sana kukabidhiwa jezi hiyo kwani itamfanya akumbuke kazi kubwa iliyofanywa na Cannavaro wakati anatumia hivyo atakuwa na nguvu ya kufanya kazi kubwa.

 

“Ninafuraha kubwa sana kukabi­dhiwa hii namba 23 kwani Cannavaro ni mtu ambaye ninamuheshimu sana na nimejifunza mengi kupitia yeye, hivyo mashabiki wa Yanga wategemee kazi mzuri zaidi kutoka kwangu.

“Nitafanya kazi kubwa sana ili mashabiki wasione pengo la beki huyo,” alisema Ninja

Comments are closed.