Haji Manara Awapa Makavu Mashabiki wa Simba

 

Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara.

Msemaji wa klabu ya Simba mwenye mbwembwe nyingi miongoni mwa klabu za soka nchini, Haji Manara, ameibuka kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuwapa makavu mashabiki wa Simba wanaoponda ushindi wao bao 1-0 dhidi ya Prisons walioupata jana uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar katika mchezo uliofungua pazia la Ligi Kuu mwaka huu.

 

Alichokisema:-

Wakati mwingine najiuliza nn wanadaamu wanataka?hasa washabiki wa Mpira!!

Nimetalii kdogo kwenye magroup machache ya Wanasimba kwenye WhatsApp nimeshangaa baadhi yetu kutokuridhika na ushindi wa leo wa goli moja dhidi ya Prisons

 

Wengine kwenye Instagram wanafika mbali zaidi eti mfumo wa kocha haufai!!

 

Guys mpira ni sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini au daktari kumfanyia upasuaji wa kichwa mtu,ukubwa wa Sayansi hii ni kwamba hujui mpinzani wako kajipangaje..hujui kama siku hyo wachezaji wako watacheza kwa kiwango gani lakini kubwa Sayansi hii haina jawabu la moja kwa moja kama hesabu au hisabati 3×3 ni tisa tu, hata ukokotoe vipi! Huku kwetu kwenye ndiki 3×3 inaweza kuwa bilioni nane.

 

Mara nyingi huwa nakataa kuwepo kwenye groups za WhatsApp sababu asilimia kubwa mpira wameujulia mitandaoni..hawana shibe ya mchezo huu adhimu kabisa!!

 

Kwao hudhani kila siku Simba itashinda na kwao ushindi ni lazma upate goli saba au tano..kwao ushindi ni mnono tu..hata kama unakutana na Wanaume wenzako!

 

Wanabeza huku wakisahau Prisons iliingia top four Msimu uliopita,wanabeza huku wakijua Prisons haifungwi kitoto kama Mnyela United!

Halaf wanakuja na hoja dhaifu inayopaliliwa na wanazi wa nazi chai eti team imetoka Uturuki why ishinde moja? Afana aleik!!

 

Hapo ndio Haji naonekana mtata aliowaambia tulienda Uturuki kujifunza mpira ni nani? Kule tulienda camp ya pre season.ni mazoezi ya mwanzo wa msimu
Wengine walienda Zanzibar kama Prisons na wapo walioenda hadi Mkamba kote huko ilikuwa inatafutwa chemistry ya timu toka kwa makocha.

 

Ni lazima mnapoamua kuushabikia mchezo huu mjifunze sayansi yake na msijifunze sayansi hii kiwepesi wepesi kama mnajifunza Sayansi kimu

 

Leo tumecheza na team nzuri na walijiandaa kama tulivyojiandaa sisi na lazma muelewe mfumo wa kocha hauingii kwa kipindi kifupi, unachukua muda kdogo

 

Niwasihi sana Wanasimba Soka ni zaidi ya mchezo wa drafti au Chess ya kina kasparov na karpovi nahitaji shabiki kabla ya kulaumu ajue vtu vingi kdogo kwenye medula yake, vinginevyo ni kufanya uchale tu.

 

Sina maana tunakataa ushauri ila uwe ushauri unaoendana na taaluma na kama huna jijengee busara ya kupiga kimya, usifate mkumbo wa mitandaoni

 

Mwisho niwasihi tena na tena cc washabiki kazi yetu ni mbili tu, sapoti na Dua na Sala, mengine ni kujitafutia kisukari kama si Pepopunda!

Salaam wakati mwingine najiuliza nn wanadaamu wanataka?hasa washabiki wa Mpira!! Nimetalii kdogo kwenye magroup machache ya Wanasimba kwenye WhatsApp nimeshangaa baadhi yetu kutokuridhika na ushindi wa leo wa goli moja dhidi ya Prisons!! Wengine kwenye Instagram wanafika mbali zaidi eti mfumo wa kocha haufai!! Guys mpira ni sayansi kubwa kuliko kwenda mwezini au daktari kumfanyia upasuaji wa kichwa mtu,ukubwa wa Sayansi hii ni kwamba hujui mpinzani wako kajipangaje..hujui kama siku hyo wachezaji wako watacheza kwa kiwango gani lakini kubwa Sayansi hii haina jawabu la moja kwa moja kama hesabu..hisabati 3×3 ni tisa tu..hata ukokotoe vipi! Huku kwetu kwenye ndiki 3×3 inaweza kuwa bilioni nane Mara nyingi huwa nakataa kuwepo kwenye groups za WhatsApp sababu asilimia kubwa mpira wameujulia mitandaoni..hawana shibe ya mchezo huu adhimu kabisa!! Kwao hudhani kila siku Simba itashinda na kwao ushindi ni lazma upate goli saba au tano..kwao ushindi ni mnono tu..hata kama unakutana na Wanaume wenzako! Wanabeza huku wakisahau Prisons iliingia top four Msimu uliopita,wanabeza huku wakijua Prisons haifungwi kitoto kama Mnyela United! Halaf wanakuja na hoja dhaifu inayopaliliwa na wanazi wa nazi chai eti team imetoka Uturuki why ishinde moja? Afana aleik!! Hapo ndio Haji naonekana mtata..aliowaambia tulienda Uturuki kujifunza mpira ni nani? Kule tulienda camp ya pre season.ni mazoezi ya mwanzo wa msimu Wengine walienda Zanzibar kama Prisons na wapo walioenda hadi Mkamba..kote huko ilikuwa inatafutwa chemistry ya team toka kwa makocha. Ni lazma mnapoamua kuushabikia mchezo huu mjifunze sayansi yake na msijifunze sayansi hii kiwepesi wepesi kama mnajifunza Sayansi kimu Leo tumecheza na team nzuri na walijiandaa kama tulivyojiandaa cc..na lazma muelewe mfumo wa kocha hauingii kwa kipindi kifupi..unachukua muda kdogo.. Niwasihi sana Wanasimba Soka ni zaidi ya mchezo wa draft au Chess ya kina kasparov na karpov..inahitaji shabiki kabla ya kulaumu ajue vtu vingi kdogo kwenye medula yake..vinginevyo ni kufanya uchale tu Sina maana tunakataa ushauri ila uwe ushauri unaoendana na taaluma na kama huna jijengee busara ya kupiga kimya..usifate mkumbo wa mitandaoni

A post shared by Haji S. Manara (@hajismanara) on

Loading...

Toa comment