The House of Favourite Newspapers

Manara Azungumzia Simba Kumtimua Kocha Masoud Djuma

Msemaji wa klabu ya Simba,  Haji Manara (kushoto) akiwa na Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma.

MSEMAJI wa klabu ya Simba, Haji Manara, amezungumzia na kupuuza uvumi uliozagaa kwamba klabu hiyo inataka kuachana na  kocha wake msaidizi, Masoud Djuma, kwa madai kwamba anatengeneza migogoro kati ya wachezaji na makocha wakuu wa klabu hiyo.

Akiandika kwenye akaunti yake ya Instagram, Manara ameeleza ifuatavyo:

”Nimepigiwa cm nyingi toka kwa waandishi wa habari na washabiki wa Simba kutaka kujua ukweli wa taarifa zilizoandikwa kwenye gazeti moja likidai kocha msaidizi wa Simba anaondoka baada ya kutofautiana na kocha Mkuu Patrick Aussems.

Kocha huyo Masoud Djuma inaarifiwa pia eti amekosana na baadhi ya wachezaji wetu.

Cm hzo zimeambatana na msg nyingi za WhatsApp na sms pamoja na kwenye page yangu ya Instagram.

Hakuna niliyemjibu zaidi ya kuchukizwa na tabia ya baadhi ya watu kukubali kila porojo inayoandikwa ama kwenye baadhi ya magazeti au mitandaoni!! Ieleweke hakuna atakaekaa Simba milele c Masoud au Aussems na hata mm ninaendika hii makala fupi,lakini wote tutaondoka pale muda wetu utakapofika na kwa utaratibu maalum Sasa huku kwenye michezo..bado kuna dhana potofu Mwandishi anaweza kuandika lolote na chochote anachojisikia bila kuulizwa wala kuchukuliwa hatua na ndio maana leo story za kupikwa zimekuwa nyingi kupita maelezo

 

Na umezuka mtindo inapikwa story kisha ndio unaulizwa eti ili ubalance story!!🤣 Haji huwa hahangaiki na kubalance porojo na hekaya..Haji anashughulikia mambo ya msingi ya maendeleo ya Taasisi

Na ukitaka kuamini hzo cooked stories zote hazina sources zinawekwa kusudi kwa dhamira zao..na hazibalansiwi kwanza..zinaandikwa kisha ndio tunaulizwa!! Narudia tena na tena kabla ya kupika hzo porojo ni vema mkabance kwanza kama taaluma inavyotaka kuliko kuandika kisha mwandishi wa gazeti hilo hilo anataka kubalance!! Na kwa mashabiki wetu c kila kinachotoka migodini ni madini mengine ni michanga tu kama iliyopo ardhini,walau ingekuwa Makanikia!! Nimalizie kwa kuwaambia Simba ni shwari na kilichoandikwa ni hekaya na hadithi sawa na zile za Abunuwasi..tusitolewe mchezoni kirahisi rahisi..tuendelee kuwa wamoja na tusiyumbishwe kwa maneno ya mahotelini
Mkata Vimeo
De Le Boss ”

Comments are closed.