The House of Favourite Newspapers

KESI YA AKINA AVEVA, ‘KABURU’ JARADA LAO BADO LIPO KWA DPP

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  jijini Dar es Salaam, upande wa utetezi umeomba iwafutie mashtaka  aliyekuwa rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ kwa sababu upande wa mashtaka umeshindwa kuiendesha kesi hiyo.

 

 

Wakili wa utetezi Nehemiah Nkoko ameyasema hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Thomas Simba baada ya Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai kueleza mahakamani hapo kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na kwamba bado wanasubiri kwa muda wa wiki tatu, Mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kwani yupo katika harakati ya kuanzisha ofisi mpya jijini Dodoma hivyo hajapata muda wa kupitia jalada hilo.

 

 

Hakimu Simba alikubaliana na maombi ya Jamuhuri na kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 14, mwaka huu ambapo upande wa mashtaka utajibu hoja za upande wa utetezi.

 

 

Katika kesi hiyo upande wa mashtaka upo katika  mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka kwa kuwaondoa washtakiwa zacharia Hans  Poppe  na Franklin Lauwo ili kesi iweze kuendelea kwa Evans Aveva na Godfrey Nyange.

 

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 10 yakiwemo ya kula njama, kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi,  kutoa maelezo ya uongo na utakatishaji fedha haramu.

 

Comments are closed.