The House of Favourite Newspapers

WAFANYAKAZI NMB WAFANYA USAFI SOKO LA FERI

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd (anayekabidhi)  akimkabidhi Mtendaji wa Soko la Samaki Feri, Mkuu Hanje (anayepokea kulia) vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi katika soko hilo.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam wakishiriki kufanya usafi katika soko la Feri lililopo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Mkoa wa Dodoma wakitoa msaada kwenye wodi ya akinamama Kituo cha Afya cha Makole cha jijini Dodoma walipofika hapo mwishoni mwa wiki kufanya usafi pamoja na kutoa misaada ya vitu mbalimbali.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Mkoa wa Dodoma wakitoa msaada kwenye wodi ya akinamama Kituo cha Afya cha Makole.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam wakishiriki kufanya usafi katika ufukwe wa soko la Feri lililopo jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam wakishiriki kufanya usafi katika  soko la Feri lililopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya NMB Makao Makuu jijini Dar es Salaam wakijitolea kufanya usafi eneo la Coco Beach Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB wakiendelea na usafi eneo la ufukwe wa coco.
Wafanyakazi wa Benki ya NMB Wilaya ya Kyela Mkoa wa Mbeya wakishiriki kufanya usafi katika eneo la kituo cha mabasi.

 

WAFANYAKAZI wa Benki ya NMB  jana walijitokeza kufanya usafi pamoja na jamii maeneo mbalimbali hapa nchini na   kutoa msaada wa vitu kwa wahitaji na vifaa vya kufanyia usafi katika baadhi ya maeneo ikiwemo soko la feri.

 

 

Kwa jijini Dar es Salaam wafanyakazi hao wakiongozwa na viongozi waandamizi wa benki hiyo walifanya usafi eneo la Coco Beach pamoja na Soko la Samaki la Feri kwa kushirikiana na wananchi waliojitokeza kufanya usafi kwenye maadhimisho ya usafi duniani.

 

 

Hata hivyo mbali na kufanya usafi katika Soko la Feri walitoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika soko hilo, ikiwa ni kuhamasisha usafi kwa jamii na kuunga mkono shughuli hizo ambazo ni muhimu kwa jamii yoyote.

 

 

Akikabidhi vifaa vya kufanyia usafi Soko la Feri, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Badru Idd alisema huo ni utaratibu wa kawaida wa benki hiyo kujitolea ama msaada au kushiriki moja kwa moja katika shughuli za kijamii ili kujenga ushirikiano kwa jamii wanayoihudumia.

 

 

Alisema Soko la Feri linahudumia watu mbalimbali ambao ni wateja wa Benki hiyo hivyo wana kila sababu kusaidia kuboresha huduma katika soko hilo. Vifaa alivyokabidhi kwa uongozi wa Soko hilo mara baada ya kuwasili ni pamoja na mifagio, reki, makoleo, mifuko maalum ya kuhifadhia na kuzolea taka na vifaa vya kujikinga wakati wa kufanya usafi.

 

 

Wakati zoezi hilo likifanyika Dar es Salaam na mikoa mbalimbali pia wafanyakazi wa Benki hiyo walifanya usafi maeneo mbalimbali pamoja na kutoa misaada kwa wahitaji hasa wagonjwa hospitalini.

 

 

Mkoani Dodoma wafanyakazi wa benki hiyo mbali na kufanya usafi walitembelea wodi ya akinamama Kituo cha Afya cha Makole na kutoa misaada mbalimbali kwa wagonjwa kituoni hapo. Mkoani Mbeya wafanyakazi walifanya usafi katika vituo vya mabasi pamoja na eneo la Kasumulo mpaka wa Tanzania na Malawi.

 

Comments are closed.