The House of Favourite Newspapers
gunners X

SSRA YAWATAKA WAFANYAKAZI KUELEWA HAKI ZAO ZA MFUKO WA FIDIA

Kaimu Mkurugenzi wa Utafiti Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini (SSRA) Joseph Mutashubilwa, (aliyesimama), akitoa hotuba kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa viongozi na watendaji wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE).

 

 

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti Sekta ya Hifadhi ya Jamii Nchini (SSRA) Dkt. Irene Isaka, amewataka viongozi na watendaji wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) kuhakikisha wanachama wao wanafahamu wajibu na haki zao katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF).

 

 

Dkt. Isaka ameyasema hayo katika hotuba ya ufunguzi wa mafunzo ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi kwa viongozi na watendaji wa TUGHE taifa na mikoani kwa niaba yake na Mkurugenzi wa Utafiti na Tathmini SSRA, Joseph Mutashubilwa mjini Morogoro Jumatatu Oktoba 1, 2018.

 

“Kwa kufanya hivi tutakuwa tunaepusha migogoro na tunadumisha mahusiano sehemu za kazi hali itakayowavutia wawekezaji kuja nchini kwa wingi na hivyo kutimiza dhamira ya Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda,” alsiema Dkt. Isaka.

 

Dkt. Isaka pia amewataka washiriki hao wa mafunzo kusambaza elimu watakayoipata kwa kuwatembelea na kuwapa elimu wanachama wa chama hicho na kumtaka kila kiongozi au mtendaji aliyeshiriki awe na mpango kazi utakaoonesha idadi ya wanachama alionao katika eneo lake na namna atakavyowafikishia elimu hii ambayo ni muhimu kwao kuifahamu.

 

 

“Nina imani kwa kufanya hivi tutakuwa tumewasaidia kwa kiasi kikubwa wanachama wetu kuujua Mfuko, kazi zake na pia kufahamu nini wanapaswa kufanya baada ya kupata matatizo wakati wakiwa wanatekeleza majukumu ya mwajiri,” alifafanua.

 

Akinukuu kifungu cha 72 (4) cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, Mkurugenzi Mkuu huyo wa SSRA alisema kifungu hicho chan sheria kinatamka nafasi ya uwakilishi wa vyama katika kamati za afya na usalama mahali pa kazi ambapo mwajiri anatakiwa kutunza kumbukumbu hizo na kamati inatakiwa kukagua ili kuona kama hilo linafanyika.

 

 

Hayo yote ni katika kuhakikisha kwamba upo ushirikishwaji wa baina viongozi  au watendaji na Serikali katika kulinda afya za wafanyakazi sehemu za kazi.

 

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uendeshaji WCF, Anselim Peter alisema, semina hiyo ya mafunzo ni muendelezo wa hatua ya Mfuko kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ambayo ni wadau wa Mfuko na nia kubwa ni kuwajengea uelewa wa madhumuni ya kuanzishwa kwa Mfuko, Sheria na jinsi Mfuko unavyofanya kazi.

 

 

Alisema katika kipindi cha miaka miwili tangu Mfuko uanze kutekeleza majukumu yake, kumekuwepo na mafanikio makubwa ya kutimiza jukumu kuu la kuanzishwa kwa Mfuko la kupokea madai na kulipa fidia na hadi sasa Mfuko tayari umekwishalipa fidia zaidi ya shilingi bilioni 4.4.

 

Naye Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Hery Mkunda, yeye alisema, mafunzo hayo yatawezesha kuongeza uelewa kuhusu wajibu wa mwajiri na haki kwa mfanyakazi katika kuelewa sheria hiyo ya Fidia.

 

“Washiriki hawa ambao ni Makatibu wa Mikoa wa TUGHE ambao wao ndiyo husimamia haki na maslahi ya wafanyakazi sehemu zao za kazi kuhakikisha wafanyakazi wanapata haki zao kwa mujibu wa sheria,” alisema.

 

Comments are closed.