MTANDAO wa simu za mkononi Vodacom Tanzania imewakumbuka baadhi ya wateja wake waliojiunga siku ya kwanza na ya pili wakati mtandao huo ukianza kazi nchini Tanzania.
Wateja hao wamepata fursa ya kutembelea shughuli mbalimbali zinazofanywa Makaao Makuu ya Ofisi za Vodacom Tanzania, kupewa zawadi pamoja na kupata fursa ya kuzungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Ndugu Hisham Hendi.
Akizungumza mara baada ya wateja hao kukabidhiwa zawadi mbalimbali, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ndugu Hisham Hendi aliwashukuru wateja hao kwa kuwa bega kwa bega na mtandao huo tangu kuanzishwa kwake na kuwahakikishia kampuni hiyo itaendelea kubuni huduma bora na nafuu kwa wateja wake.
Aidha aliwataka kuwa mabalozi wazuri wa Vodacom Tanzania kwa kuwa wao wamejifunza mengi kwa kutembelea shughuli za mtandao huo na kupata fursa ya kuuliza masuala mengi yanayofanywa na mtandao huo unaoongoza wa simu za mkononi nchini Tanzani.
“Tunawashukuru sana kwa kuwa na Vodacom tangu inaanzishwa hadi leo naomba muendelee kuwa mabalozi wetu, kwa mlichojifunza leo,” alisema Hisham Hendi.
Katika tukio hilo, Hendi pia aliwahudumia wateja na kukata keki maalum kabla ya kuanza kuwagawia wateja wake waliokuwa wakiendelea kupata huduma kwenye duka la Vodacom na kituo cha huduma kwa wateja cha kampuni hiyo kilichopo Makao Makuu ya Ofisi za Vodacom Barabara ya Kawawa, Jijini Dar es Salaam.
Comments are closed.