The House of Favourite Newspapers

Simba Wamfuata Ajibu

Ibrahim Ajibu

MENEJA wa straika kipenzi cha mashabiki wa Yanga, Ibrahim Ajibu ameweka wazi kwamba mteja wake anatakiwa na Simba.

Ajibu ambaye anavaa jezi namba kumi, alijiunga na Yanga msimu wa 2017/18 akitokea Simba, lakini hakufanya makubwa kama alivyoanza msimu huu, mwaka jana alimaliza akiwa na mabao saba pekee.

 

Msimu huu amehusika kwenye mabao nane kati ya 11 ambayo Yanga imeyafunga mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara.

Katika mabao hayo, Ajibu amefunga mawili na kutoa pasi sita za mabao. Amefanya hivyo katika mechi sita za ligi alizo­cheza mpaka sasa.

 

Meneja huyo wa Ajibu aju­likanaye kwa jina la Athumani Ajibu ambaye ni kaka yake, ameliambia Spoti Xtra kuwa kwa sasa kiwango cha mdogo wake kimewavutia zaidi ya timu tano ikiwemo Simba.

 

“Kutokana na uwezo ambao anauonyesha Ajibu, viongozi wa Simba wamenifuata ili ni­weze kuzungumza nao kwani hata msimu uliopita kabla hajajiunga na Yanga waliniam­bia kuwa bado wanahitaji saini yake ila tulishindwana bei,” alisema meneja huyo ambaye mteja wake kuanzia mwezi Desemba atakuwa huru kwa mazungumzo na klabu yoyote.

 

“Viongozi wa Simba wa­menifuata ili kuweza kujua namna gani tunaweza ku­fanya makubaliano, hata Ajibu mwenyewe aliniambia kuwa amekuwa akiwasiliana na viongozi hao wakimpongeza na kuonesha nia ya kumrejesha ila nimemwambia aongeze juhudi kwa kuwa bado ana mkataba na timu yake ya Yanga,” al­iongeza ingawa Spoti Xtra linajua Yanga nao wameanza kujipanga kumpa mkataba mpya.

 

“Kwa kuwa hivi sasa bado ni mali ya Yanga, hivyo hawezi kujiunga na timu nyingine,” alisema meneja huyo.

Wakati Ajibu anasaini Yanga mkataba wa miaka miwili, alik­abidhiwa dau la Sh milioni 70, gari na nyumba ya kuishi ikiwa ni sehemu ya mkataba huo ambao mwishoni mwa msimu huu unamalizika.

 

Mchezaji huyo amekuwa gumzo wiki hii kutokana na goli lake la tiktak alilofunga dhidi ya Mbao jijini Dar es Salaam kusambaa kwenye mitandao ya kijamii.

STORI NA LUNYAMADZO MLYUKA

Comments are closed.