The House of Favourite Newspapers

MKUU WA MAJESHI JWTZ AIPONGEZA NMB KUKUZA MCHEZO WA GOLF

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakub Mohamed (wa pili kulia)  akimkabidhi kikombe mshindi wa jumla katika mashindano hayo, Richard Mtweve (kulia).
Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakub Mohamed akizungumza jambo.

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard (kushoto) akimkabidhi zawadi mmoja wa washindi katika Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf yaliyofanyika kwenye Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa jumla katika Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf, Richard Mtweve akizungumza jambo.
Rais wa Chama cha Mchezo wa Golf  Tanzania (TGU), Chris Martin (kuliaa) akimkabidhi kitabu cha mwongozo wa mchezo wa golf Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard ili naye aendelee kuwa mdau wa mchezo huo.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya NMB, Donatus Richard (kulia) akiitambulisha timu ya NMB kwenye hafla hiyo.
Mmoja wa wachezaji katika Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf akiendelea na mchezo.
Rais wa Chama cha Mchezo wa Golf  Tanzania (TGU), Chris Martin (kulia) akimkabidhi kitabu cha mwongozo wa mchezo wa golf Mkuu wa Majeshi mstaafu, Jenerali Mirisho Sarakikya (kushoto) ambaye ni mchezaji wa mchezo huo. 

 

 

MKUU wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo ameipongeza Benki ya NMB nchini kwa juhudi zake za kuendelea kuukuza mchezo wa Golf Tanzania.

 

 

Jenerali Mabeyo ametoa pongezi hizo jana kupitia kwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali Yakub Mohamed alipokuwa akimwakilisha katika hafla ya kufunga Mashindano ya NMB Kombe la Mkuu wa Majeshi kwa mchezo wa Golf yaliyofanyika kwenye Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo jijini Dar es Salaam.

 

 

Akizungumza kwa niaba ya Jenerali Mabeyo, Luteni Jenerali Mohamed alisema jamii ya mchezo wa Golf Tanzania inatambua mchango mkubwa unaotolewa na NMB katika kudhamini mchezo huo mara zote jambo ambalo linaendeleza kukua kwa mchezo huo nchini, hivyo wataendelea kushirikiana na benki hiyo.

 

 

Alisema NMB wamedhamini mashindano hayo kwa mwaka wa tatu mfululizo huku yakizidi kukua na mchezo huo kuwa maarufu nchini, na yamekuwa yakishirikisha wachezaji vijana na wameanza kufanya vizuri jambo ambalo ni mafanikio kwa taifa kimichezo.

 

Akizungumza katika hafla hiyo, mwakilishi wa NMB alisema benki hiyo itaendelea kushirikiana na jamii katika kuendeleza na kukuza michezo yote pale inapopata fursa kwani mbali ya kujenga mahusiano mazuri na jamii pia ni afya na sasa ni sehemu ya ajira kwa jamii. Alisema NMB itaendelea kushirikiana na Klabu ya Golf ya JWTZ Lugalo kwani ni shukrani kwa mahusiano waliyonayo kikazi.

 

 

Aidha aliwakaribisha maofisa wa juu na wateja wengine maalum kuungana katika kujipatia huduma za kibenki zinazotolewa kwao kama wateja maalum ikiwemo mikopo nafuu na ya haraka, ushauri wa kifedha na kadi maalum za kupata huduma za kibenki popote.

 

 

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Mchezo wa Golf  Tanzania (TGU), Chris Martin alisema chama hicho kimejipangia kufikisha wachezaji 3000 wamchezo huo ifikapo 2020, huku idadi ya wachezaji kwa sasa haifiki 1000.

 

Alisema Klabu ya Golf Lugalo imekuwa ikifanya vizuri kwani hadi sasa inawachezaji vijana (watoto) takribani 60 na 22 kati yao wameshiriki katika Kombe la NMB Mashindano ya Golf ya Mkuu wa JWTZ, jambo ambalo linaleta matumaini ya kuendelea kukua kwa mchezo huo.

 

 

Washindi katika mashindano hayo, yalioshirikisha wachezaji wa ridhaa 79, wakulipwa 19 na watoto 22 walijipatia fedha taslimu, vikombe na zawadi za vifaa mbalimbali kama friji, TV, radio, baskeli, dish za ving’amuzi na vinginevyo.

 

 

NMB ilidhamini mashindano hayo kwa kuchaangia shilingi milioni 26 pamoja na vifaa mbalimbali zikiwemo jezi zilizotumiwa katika mashindano hayo.

 

 

 

 

Comments are closed.