The House of Favourite Newspapers

Hans Poppe Aachiwa Kwa Dhamana

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba, Zakaria Hans Poppe (katikati),  akiongea na Godfrey Nyange maarufu Kaburu (wa pili kutoka kulia) na aliyekuwa rais wa Simba, Evans Aveva (kulia).

MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili wa Klabu ya Simba, Zakaria Hans Poppe,  ameachiwa kwa dhamana ya Sh. mil.  15 ambapo  kesi yake itatajwa Ijumaa.

Poppe alifikishwa kwa mara ya kwanza katika mahakama hiyo saa tatu na nusu na kupelekwa moja kwa moja katika chumba cha mahabusu akisubiri kupandishwa kizimbani

Awali upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shedrack Kimaro, uliomba kumuunganisha Poppe katika kesi inayowakabili aliyekuwa rais wa Simba, Evans Aveva na aliyekuwa makamu wake, Godfrey Nyange maarufu Kaburu.

 

Hata hivyo, upande wa utetezi ukiongozwa na Wandiba ulipinga ukidai kuwa mahakama ilishatoa uamuzi kuwa kesi iendelee kwa washtakiwa waliopo mahakamani na kwamba kwa maombi hayo, mahakama ina lengo la kirudisha nyuma kesi hiyo.


Hivyo, Wandiba ameomba mahakama hiyo iendelee na kesi dhidi ya washtakiwa waliopo mahakamani na Poppe afunguliwe mashtaka yake.

 

Hakimu Mkazi Mkuu anayesikiliza shauri hilo, Thomas Simba, baada ya kusikiliza hoja za pande zote, alibidi aandike uamuzi ama kukubiliana na upande wa mashtaka wa kumuunganisha Poppe katika kesi ya akina Aveva au kutupilia mbali maombi hayo ya upande wa mashtaka.

 

Comments are closed.