The House of Favourite Newspapers

Mkude Majeruhi, Aipa Presha Simba

Kiungo wa Simba, Jonas Mkude.

 

KIUNGO wa Simba, Jonas Mkude huenda akaukosa mchezo ujao dhidi ya Stand United licha ya kuanza mazoezi mepesi jana Alhamisi kutokana na kuuguza majeraha ya nyama za paja.

Mkude alipata matatizo hayo akiwa na timu ya taifa, Taifa Stars na kushindwa kucheza michezo yote mwili nyumbani na ugenini dhidi ya Cape Verde.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema kiungo huyo kwa sasa anafanya mazoezi mepesi kwanza ili kuweza kuangalia hali yake.

 

“Mkude anaendelea vizuri tofauti na awali na suala la mazoezi anaanza leo (jana Alhamisi) mazoezi yale mepesi kwa ajili ya kumuangalia kama anaweza kuungana na wenzake.

“Kuelekea mchezo wa Jumapili sina hakika kama anaweza kucheza au asicheze, hilo litategemea na hali yake pamoja na maamuzi ya kocha kwamba ampange au vipi lakini wachezaji wengine wote wapo fiti,” alisema Gembe.

 

Ikumbukwe kwa sasa mchezaji wa Simba ambaye ni majeruhi ni Salim Mbonde ambaye yupo nje kwa zaidi ya miezi mitano sasa.

Stori na Martha Mboma | Championi Ijumaa

JPM “INASIKITISHA Mnapigwa 3/ Viongozi Wezi Mnakula Fedha”

Comments are closed.