USIKU WA MWAMBAO DAR LIVE, HIVI NDIVYO KILIVYONUKISHWA!

Wanamuziki wa First Class wakiwajibika jukwaani.

 

USIKU wa kuamkia leo wapenzi wa burudani waliofurika ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live huko Mbagala-Zakhem, walipata uhondo bab’kubwa kwenye onyesho la Usiku wa Mwambao lililokutanisha miamba ya muziki na kusindikizwa na burudani zingine kama vile muziki wa Singeli kutoka kwa Sholo Mwamba na Kibao Kata kutoka kwa mkali wa kuchagiza almaarufu kwa jina la Kivurunde.

Maua (wa pili kushoto) akicheza na mashabiki walioshindwa kujizuia na kumvamia jukwaani.

Burudani hiyo iliwafanya mashabiki wapagawe na kujimwaya uwanjani mwanzo-mwisho huku  zikichezwa staili mbalimbali zilizokuwa zikinogesha usiku huo.

Mashabiki wakiwa wamekolezwa na uhondo.

Makundi yaliyotoa burudani kwenye onyesho hilo ni First Class linaloongozwa na Athuman Sudi a.k.a Amigo; Ogopa Kopa linaloongozwa na Malkia wa Mipasho, Khadija Khopa; Yah TMK linaloongozwa na Omary Tego na dada yake Maua Tego,  na vikundi vingine vya burudani.

Aisha Vuvuzela wa Ogopa Khopa akiwajibika mbele ya mashabiki.

Khadija Kopa na Amigo wakiimba kibao chao kipya walichoshirikiana.

Khadija (katikati) akienda sambamba na kundi lake kwa staili iliyowaacha hoi mashabiki.

Mkali wa Singeli, Sholo Mwamba,  naye akiliamsha dude ukumbini hapo.

PICHA: RICHARD BUKOS | GPL


Loading...

Toa comment