The House of Favourite Newspapers

Spika Ndugai Apongeza NMB Kutoa Elimu ya Ujasiriamali Kwa Watanzania

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akifungua jumuiko la wateja wa Benki ya NMB lililofanyika jijini Dodoma.
Afisa Mkuu wa Mikopo kutoka Benki ya NMB, Tom Borghols, akizungumza jambo katika hafla hiyo.
Viongozi wakiendelea kuzungumza jambo katika hafla hiyo.
Baadhi ya wajasiriamali 300 wa Mkoa wa Dodoma ambao ni wafanyabiashara wa club za wafanyabiashara (NMB Business Club) wa Benki ya NMB walioshiriki.
Hafla ikiendelea.
Washiriki wakifuatilia kwa makini kilichokuwa kikiendelea mbele.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na   washiriki wa  club za wafanyabiashara (NMB Business Club) wa Benki ya NMB jijini Dodoma.

 

 

Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuwa watanzania wengi wamekuwa wakishindwa kufikia malengo yao kutokana na kutokuwa na elimu ya ujasiriamali na hivyo pesa wanazokopa kushindwa kuzifanyia malengo waliyokusudia.

 

Kutokana na kuwepo kwa hali hiyo, Mh. Ndugai ameitaka Benki ya NMB kuhakikisha inatoa elimu ya ujasiriamali ili kuwawezesha wananchi kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

 

Spika ametoa kauli hiyo jijini dodoma wakati alipokuwa akifungua jumuiko la wateja wa Benki ya NMB lengo likiwa ni kutoa elimu za biashara na namna ya kutunza fedha.

 

Aidha Spika ameipongeza Benki ya NMB kwa kuandaa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyabiashara, kwani elimu hiyo ni muhimu katika kuwajengea uwezo wafanyabiashara na wananchi juu ya umuhimu wakulipa kodi na kujenga mahusiano mazuri na wadau na taasisi mbalimbali za umma.

 

Naye Afisa Mkuu wa Mikopo, Tom Borghols amesema kuwa hivi sasa benki hiyo imeboresha utoaji wa huduma zake ikiwa ni pamoja na kuondoa baadhi ya masharti hasa ya hati ya nyumba kwa wateja wanaotaka kukopa mikopo mikubwa pamoja na kumpa mamlaka meneja wa tawi kuidhinisha mkopo kwa mteja hadi wa shilingi milioni 50.

 

Jumuiko hilo lililoandaliwa na benki hiyo ya nmb limewashirikisha jumla ya wajasiriamali 300 wa mkoa wa Dodoma ambao ni wafanyabiashara wa club za wafanyabiashara (NMB Business Club) wa Benki ya NMB jijini hapo .

Comments are closed.