Mburkinafaso Kuanza na Staili yake Simba

Burkinafaso, Zana Coulibaly.

BEKI mpya wa Simba raia wa Burkinafaso, Zana Coulibaly amesema kuwa ana deni kubwa la kulilipa katika timu hiyo baada ya kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo.

 

Simba ilimsainisha mkataba wa miaka miwili beki huyo aliyekuja kuchukua nafasi ya Shomari Kapombe aliyevunjika mfupa wa enka wakati akiwa kwenye kambi ya Taifa Stars kabla ya kuwavaa Lesotho katika mchezo wa kuwania kufuzu Afcon.

 

Beki huyo amesajiliwa na Simba baada ya Kocha Mkuu wa timu hiyo Mbelgiji, Patrick Aussems kupendekeza asajiliwe haraka ili amtumie kwenye michezo ijayo ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Coulibaly alisema; “Ninajivunia kuwepo kwenye timu hii kubwa iliyokuwa na umoja, ushirikiano huku ikipata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wake ambao nimewaona uwanjani ilipocheza Mbabane.”

 

“Hivyo, baada ya kusaini mkataba niseme kuwa nina deni kubwa la kulilipa Simba na hakuna cha kuwalipa zaidi ya furaha ya kuchukua makombe yote tunayoshiriki,” alisema Coulibaly.

Toa comment