The House of Favourite Newspapers

Siri Ya Mabao Ya Makambo Yafichuka

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ameitaja siri ya mshambuliaji wa timu hiyo, Heritier Makambo kuwa na kiwango kizuri kwa sasa.

 

Zahera ambaye ni raia wa DR Congo kama ilivyo kwa Makambo, alisema kitendo cha yeye kumsema Makambo kila kukicha ndiyo sababu kubwa iliyo­mfanya mshambuliaji huyo kuwa na makali zaidi kwa sasa.

Makambo ambaye amejiunga na Yanga msimu huu, alianza taratibu lakini kasi yake imeongezeka akiwa amefunga mabao nane katika Ligi Kuu Bara.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Zahera alisema: “Kuna kipindi nilikuwa namsema sana kutokana na kucheza chini ya kiwango, hali hiyo kwa sasa imemfanya awe bora.

 

“Si hivyo tu, pia amepunguza kupu­uza mazoezi na sasa anazingatia kila kitu jambo ambalo linamfanya azidi kuwa bora.”

 

“Nilimzungumza vibaya kwa kuwa nilikuwa najua kabisa kuna vitu Makambo anavifanya siyo vya kinid­hamu ikiwemo kutozingatia muda wa kupumzika na ratiba yake ya kula, hivyo subirieni kumuona akiendelea kufunga zaidi.”

Comments are closed.