Jinsi Ya Kuongeza Fursa Za Mafanikio Kila Siku

Miongoni mwa mambo makubwa sana niliyojifunza mwaka huu unaoelekea ukingoni kuhusiana na fursa za mafanikio maishani, ni kitu ninachokiita (referability index), ule uwezo wako wa kuaminiwa hadi kiwango cha kupendekezwa na mtu mwingine. Ukweli ni kuwa fursa si kitu kilichoko hewani bali fursa zipo katika mikono na mitandao ya watu wengine unaowafahamu na wengine usiowafahamu.

 

Mara nyingi watu huulizwa kama wanaweza kutafuta mtu wa kufanya kitu fulani (wanataja sifa). Ukweli ni kuwa kazi hii huwa ngumu sana hasa kwa kuzingatia kuwa kila unayempendekeza anabeba jina lako na akiboronga nawe utaonekana haufai ila akifanya vizuri nawe utaonekana

unafaa. Hii ndiyo sababu ya watu wengi hata makazini wakiambiwa kuna fursa, huogopa moja kwa moja kupendekeza mtu kwani inaathiri katika sifa yao pia (reputation). Hivi hujawahi kusikia watu wanatafuta MC wa harusi na mtu anatajwa kisha kila mtu anasema; ”huyo hapana kabisa” au fundi gari anasifika kwa wizi wa vifaa na kila anayetaka kupeleka gari kwake anaambiwa sifa zake mbaya au mfanyabiashara ukishamtumia pesa ni msumbufu kupindukia au mtu ni mchonganishi kwa wafanyakazi wenzake?

 

Lakini pamoja na hayo yote, wapo watu wengi ambao hata wewe ukiambiwa uwapendekeze, huwezi kuwaza mara mbilimbli kwani ni watu unawaamini sana katika maisha yako. Leo ningependa uzifahamu sifa mbili za kujijengea maishani ili uwe mtu ambaye jina lako litakuwa la kuaminika na kutajwa haraka kila fursa inayokuhusu inapotokea.

1: UWe MKWeLi nA MWAMiniFU Hakuna kitu cha hatari kama kukosa uaminifu katika majukumu unayopewa na hasa katika eneo la pesa. Kama wewe ni mtu ambaye huwezi kuaminiwa katika eneo hili, safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio itakuwa ngumu sana.

 

Kama kila wakati unajiunga na wenzako kutafuta mbinu za kuiibia ofisi pesa kupitia udanganyifu wa aina mbalimbali au unatapeli watu kwa kutumia bidhaa unazouza au kukopa na kulipa ni hadi usumbue waliokukopesha, basi uwe na uhakika hakuna atakayetaja jina lako fursa kubwa itakapokuja. Unatakiwa uzoee kusema ukweli kuliko uongo; usidanganye umechelewa kwenye foleni wakati unajua ulichelewa kutoka nyumbani, wengine wanaokuuliza wanakuona ila hawatakuambia kamwe kuwa wanakuona ila hawatakutaja jina lako kwenye fursa nyingine. Ni bora kuwa mkweli na mwaminifu kuliko kuwa muongo na ukaziba fursa zako za mbeleni.

2: KiLA UnACHoFAnYA FAnYA KWA UBoRA WA HALi YA JUU Bila kujali kama unalipwa au hulipwi, bila kujali kama unalipwa kiwango kidogo na kile unachotarajia au la. Cha muhimu ni kuwa kama umeamua kufanya jambo lolote maishani mwako, basi lifanye kwa bidii zote bila ulegevu na ulifanye kwa ubora.

 

Kanuni itakayokusaidia maishani ni kujiuliza swali hili; Kama ningeambiwa napewa pesa kiwango cha juu kabisa ninachotaka kwa masharti ya kuifanya kazi hii, je, ningeifanya hivi nilivyofanya? Kama jibu ni hapana, basi ujue unazuia fursa zako zinazofuata.

 

Usifanye jambo kwa kuangalia kile unachopata leo, bali kwa kuangalia ni fursa gani unaweza kuzifungua kesho. Bila kujali kwa leo uko katika nafasi gani na unafanya shughuli gani, fanya jambo ambalo utaongeza uwezo wako wa kuaminiwa na kutajwa kwa jina lako katika fursa zinazokuja mbele yako.

 

Kamilisha kazi ya watu uliyopewa, peleka bidhaa ambayo ilishalipiwa, usichelewe appointment makusudi ukasingizia foleni, pancha au kuuguliwa, ahidi mambo ambayo una nia ya dhati ya kuyafanya na si kufurahisha watu kisha hufanyi. Kumbuka kuwa SIFA MBAYA husambaa kwa kasi sana kuliko SIFA NZURI. Hivyo, ziepuke kabisa ili kuifikia ndoto yako. ndoto YAKo inAWezeKAnA! Kwa maoni au ushauri, tuwasiliane kwa namba hiyo hapo juu.

Loading...

Toa comment