The House of Favourite Newspapers

Uwoya Afungukia Jeuri ya Pesa

Staa wa Bongo Movie, Irene Uwoya

KUFUATIA kuonesha jeuri ya pesa kwa siku za hivi karibuni, Amani lilimbana staa wa Bongo Movie, Irene Uwoya na kumuuliza anapata wapi jeuri hiyo? Mrembo huyo amefunguka!

Uwoya ambaye hivi karibuni alifanya sherehe baab’kubwa ya kuzaliwa na kuwalisha watoto yatima, kisha kuwachukua marafiki zake na kukodi boti kwenda Zanzibar kufanya matanuzi, amesema siri ya kufuru hiyo ni biashara zake ambazo hakupenda kuzitaja.

 

“Mimi nafanya biashara na pia ninafanya matangazo nje ya nchi hivyo ndivyo vitu vinavyonipa jeuri ya kuinjoi maisha,” alisema Uwoya ambaye hivi karibuni anatarajia kuzindua upya baa yake iliyokuwa kwenye ukarabati.

STPRI NA IMELDA MTEMA, AMANI

Comments are closed.