The House of Favourite Newspapers

Kajala Ataka Kuanza Mwaka Akiwa Safi

Mkali wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja

AMANI tupu! Mkali wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ameapa kumaliza mwaka 2018, bila kugombana wala kuwa na bifu na mtu kwa sababu anataka kuanza mwaka 2019 akiwa safi.

 

Kajala aliliambia Ijumaa kuwa anamuomba mno Mungu aanze mwaka ujao akiwa hana adui na hata kama kutakuwa na mtu amemkosea, ataenda kumuomba msamaha kwa sababu anataka kufunguliwa mambo yake.

 

“Kabla ya kumaliza mwaka huu, sitaki kuwa na bifu na mtu na hata kama kuna mtu nitakuwa nimemkosea, nitamfuata mwenyewe na kutaka mwaka unaokuja tuuanze vizuri, mambo ya mabifu yanafunga bahati na mambo mazuri,” alisema Kajala.

Stori: Imelda Mtema

Comments are closed.